📖 elimu 🌑haibadili 🌎 dunia 📚 elimu 🌔 hubadili 👬🏾 watu na 👨‍👧‍👧 watu 🌏hubadili DUNIA🗼

1.26M Followers

1.26M Followers
1.26M Followers

UGA WA ELIMU

📕📕KARIBU TUSOME SASA KATIKA MAWANDA MAPANA📕📕 📕Tunarahisisha Usomaji📕Soma Kisasa📕

UHAKIKI WA NGOSWE PENZI KITOVU CHA UZEMBE NA EDWIN SEMZABA

UHAKIKI wa NGOSWE Penzi Kitovu cha Uzembe

UHAKIKI WA TAMTHILIYA YA NGOSWE – PENZI
KITOVU CHA UZEMBE
MTUNZI: EDWINI
SEMZABA
WACHAPISHAJI:THE
GENERAL BOOKSELLERS LTD
CHAPA YA 1-1988
UTANGULIZI

Ngoswe-penzi Kitvu cha Uzembe  inaonyesha namna jamii inapaswa kushiriki
mipango mbalimbali ikiwepo ya kisiasa kiuchumi na kiutamaduni.Mafanikio ya
mipango hiyo inategemea na kujulikana kwa idadi ya watu utayari,uelewa wa watu
hao kuhusu mipango husika
Tamthiliya hii inaonyeshakazi
ya kuhesabu watu ilivyokwama kijijini kwa mzee mitomingi ngengemkeni kutokana
na uzembe wa afisa wa kuhesabu sensa Ngoswe.

FANI
Vipengele vya fani katika kazi
ya fasihi ni muundo ,mtindo,madhari ,wahusika na matumizi ya lugha
MUUNDO
Muundo uliotumika katika tamthiliya
ni wamuundo
wa moja kwa moja ambapo kazi nzima ipo katika sehemu tano ambazo
mwandishi amezipa majina ya kitwasira kulingana na ukubwa wa tatizo
linalozungumziwa ,yaani ameonyesha kuingia kwa Ngoswe kijijini mazingira yanayoashiria
hali ngumu ya maisha(kijito)
Ø
Sehemu
ya pili inaonyesha kazi ya kuhesabu watu imeanza na watu hawana utayari na
uelewa juu ya sensa (vijito)
Ø
Sehemu
ya tatu inaonyesha Ngoswe ameanza kujihusisha na mapenzi na ulevi,ambavyo ni
viashiria vya kuharibu kazi yake (mto)
Ø
Sehemu
ya nne inaonyesha kazi aliyopewa Ngoswe tayari imekosa mwelekeo,Ngoswe amebobea
kwenye mapenzi na ulevi, karatasi zinachomwa moto baada ya kumtorosha Mazoea (jito)
Ø
Sehemu
ya tano inaonyesha serikali ikimuhukumu Ngoswe juu ya takwimu zilizoungua moto
na Ngoswe asingizia kuwa kijijini kuna shida ya kuhesabu kwani nyumba
zimejitenga na watu wenyewe kutoelewa (baharini)
MTINDO
Mtindo uliotumika ni wa kidayalojia
ambapo wahusika wake wanazungumza kwa kujibizana
Pia kuna matumizi ya nafsi zote
tatu na nafsi hizo zimetumika katika sehemu mbalimbali.Mfano sehemu ya tano kwa
matumizi ya nafsi ya kwanza pale Ngoswe anapoulizwa na serikali kuhusu takwimu
akajibu “usemi sinao”
MANDHARI
Kitabu hiki kimejengwa katika
mandhari ya kijijini,hii inadhihirishwa na ukosefu wa huduma muhimu kama vile
shule hospitali na miundo mbinu
Tabia za wahusika pia
zinaonyesha mandhari ya kijijini mfano,ulevi wa pombe za mnazi,watu kutojali
elimu,kun’gan’gania mila zilizopitwa na wakati
MATUMIZI YA LUGHA
Mwandishi ametumia lugha
nyepesi na yenye kueleweka pia mwandishi ametumia tamathali za semi,misemo na mbinu
nyingi za kisanaa.
Tamathali za semi
Hizi ni semi au kauli
zitumiwazo na mwandishi katika kazi ya fasihi ili kuongeza ladha katika kazi
husika
Tashibiha
Ni  tamathali ilinganishayo vitu viwili au zaidi
kwa kutumia viunganishi kama mithili ya ,kama,mfano wa
Mfano,Ngoswe anaposhangaa ardhi
ya kijijini kwa balozi Mitomingi anasema
·
Udongo
mwekundu kama ugoro wa sabiani
·
Tazama
suruali yake kama kengele ya bomani
·
Nikitoka
hapa najitupa kitandani kama gogo
Tafsida
Ni tamathali itumiwayo
kupunguza ukali wa maneno
mfano Mainda anasema labda
anajisaidia(Uk 21)
Takriri
ni tamathali inayorudiarudia
neno ili kuweka mkazo juu ya kile kinachosemwa
Mfano; karibu,karibu(pale
Ngoswe alipokuwa akikaribishwa)
Mdokezo
Ni tamathali ambayo hueleza
jambo kwa kukatakata maelezo
Mfano Mazoea anasema
sijui……sijui……siwezi namwogopa baba (Uk 22)
Tanakali za sauti
Ni tamathali inayoiga mlio wa
vitu
mfano Ngoswe alishindwa
kujizuia akacheka ha ha ha ha
Methali
Ngoswe anamwambia Mazoea
v  “Penye nia pana njia” (uk 22)
Misemo
  v
Hebu
keti tutupe mawe pangoni
  v
Kupeleka
chakula ndio unafanya makambi
Taswira/Jazanda
Taswira mbalimbali zimetumiwa
na mwandishi katika tamthiliya hii. Msanii ametumia taswira ya mtu kwa kuhusisha
na matukio ya wahusika.Mwandishi analinganisha mwanzo wa mchezo ni kijito ni
mto mdogo sana hivyo maelezo ya sehemu hii yanategemewa kuwa madogo sana
  v
Sehemu
inayofuata ya vijito,sehemu ya vijito inaonyesha kuwa masuala                  yanashughulikiwa
na kujadiliwa hapa yanaongeza uzito ingawa sio mazito sana
  v
sehemu
ya mto inaonyesha ukubwa wa shughuli ya
Ngoswe yuko kazini (yuko m toni)tayari yupo ndani ya jukwaa bila shaka maji ya mto
ni mengi (matatizo mengi)na hivyo yeyote atakayeingia mtoni yampasa awe
mwangalifu
  v
sehemu
ya jito inaashiria kuna hatari, kuna matatizo mengi, katika jito kulivika si
kazi rahisi hatimaye tunaonyeshwa Ngoswe amezama baharini ambapo kuzama kwa
Ngoswe ni baada ya makaratasi kuchomwa moto.
WAHUSIKA
Wahusika ni watu walioshiriki
katika mchezo au tamthiliya husika.
Mwandishi amegawa wahusika
katika makundi mawili yaani mhusika mkuu na wahusika wasaidizi
MHUSIKA MKUU
NGOSWE
Ni msomi anayependa kazi ya
kuhesabu watu lakini kutokana na tamaa ya mwili wake anaharibu kazi baada ya
takwimu zote kuchomwa moto na Mitomingi kutokana na kitendo cha kujaribu
kumtorosha mazoea .
WAHUSIKA WADOGO
Mazoea
  v
Msichana
mwenye umri wa miaka 18-20
  v
Ni
mtoto wa balozi (Mitimingi)
  v
Anawakilisha
wanawake wasio na msimamo katika mapenzi
Ngengemkeni mitomingi
  v
Huyu
ni balozi
  v
Baba
yake Mazoea
  v
Anachoma
karatasi za takwimu kutokana na Ngoswe kutaka kumtorosha Mazoea
  v
Ni
mzee aliyeshikilia ukale na anapenda ndoa za mitara
JINA LA KITABU
Ngoswe penzi kitovu cha uzembe
jina hilo la kitabu linasadifu yaliyomo ndani ya kitabu ,kwani msanii kwa kiasi
kikubwa amejaribu kujadili na kuonyesha matatizo yanayoikumba jamii katika
shughuli za kijamii,matatizo hayo ni kama uchawi ulevi uzembe na dhana nyingine
potofu
KUFAULU NA KUTOFAULU KWA
MWANDISHI


Mwandishi katika tamthiliya hii
amefeli kwa kuwa ameonyesha matatizo yaliyomo katika jamii bila kuonyesha mbinu
mbadala ya kuyatatua.

BOFYA HAPA KUENDELEA NA UHAKIKI WA MAUDHUI
Share:

UHAKIKI WA TAMTHILIYA YA NGUZO MAMA YA PENINA MUHANDO (Hassan Lemunje)

NGUZO MAMA 

MWANDISHI: PENINA MUHANDO
WACHAPISHAJI: DUP
MWAKA: 1982
 NGUZO MAMA ---UHAKIKI WA... - OUTSO Kinondoni. | Facebook
UTANGULIZI
Tamthiliya ya Nguzo
Mama
 iliyoandikwa na Penina Muhando inayasawiri na kuyaelezea matatizo
mbalimbali yanayowakabili na kuwaelemea wanawake wengi wa Tanzania na Afrika
kwa ujumla. Wanawake wengi wamekuwa wakinyanyasika kwa kunyanyaswa na kuteswa
na waume zao. Penina Muhando anathibitisha hayo kwa kutueleza maisha waliyokuwa
wakiishi wanawake wa Patata.

FANI
MUUNDO
Msanii ametumia muundo wa moja kwa moja. Tamthiliya
hii imeanza kuonesha jinsi nguzo mama ilivyolala na harakati za kina mama
kastika kunyanyua nguzo mama. Mchezo umegawanyika katika sehemu nne.
MTINDO
Msanii ametumia mtindo wa dayolojia na masimulizi.
Vilevile ametumia lugha ya kishairi ili kuleta mvuto katika mchezo wake. Pia
msanii ametumia nyimbo na mianzo ya hadithi za fasihi simulizi. (uk 3).
MATUMIZI YA LUGHA
MISEMO/ NAHAU
a)
Utakiona
cha mtema kuni (uk 42).
b)
Watoto
ni taifa kesho (uk 55).
c)
Utakufa
kibudu (uk 22).
d)
Akachanganya
ulimi {uk 57).
e)
Dume
Malaya si dume roho yako kusumbua (uk 40).
  METHALI
i)
La
mgambo likilia lina jambo (uk 45).
ii)
Aso
mwana aeleke jiwe (uk 45).
iii)
Umoja
ni nguvu utengano ni udhaifu (uk 33).
TAMATHALI ZA SEMI
TASHIBIHA
*Anatembea kama kapigwa bumbuazi (uk 9).
* Sikilizeni na sauti kama ndege nyikani (uk 30).
*Wanaswagwa kama mbuzi (uk 44).
*Amevaa kama mkulima wa bara (uk 24).
TASHIHISI
-Hasira zikampanda Bi Nane (uk 8).
SITIARI
-Mbwa mume wako
anayefuata wanawakeovyo.
MBINU NYINGINE ZA KISANAA
TAKRIRI
-Wakajaribu , wakajaribu (uk 5).
-Mwachie! Mwachie! Mwachie! (uk 8).
-Toka! Toka! Toka usirudi tena (uk 8).
-Akaenda, akaenda, akaenda (uk 40).
MDOKEZO
*Wakavuta…….wakavuta……….(uk 35).
*Siku moja ………ngojeni niwaoneshe (uk 49).
*Ee ndiyo malezi ya watoto wetu………(uk 52).
*Hebu tutazame kwanza kwanini hawasogei….(uk 58).
TANAKALI SAUTI
*Lu lu lu lu lu lu lu lu lu! (uk 2 na 18).
*Ai ai ai ai ai ai ai ai ai ai! (uk 2).
MATUMIZI YA KIINGEREZA
-My God  (uk 32,
49, 50).
LUGHA ZA MATUSI
-Shika adabu yako
(uk 39).
-Malaya mkubwa wewe (uk 39).
-Mbwa wee! (uk 39).
-Mbwa mume wako anayefuata wanawake ovyo (uk 39).
WAHUSIKA
  1. Bi Moja
*Mke wa Shabani
*Hakuwa na msimamo katika kusimamisha Nguzo Mama.
*Alikuwa na tama.
*Hafai kuigwa na jamii.
2. Bi Pili
*Mke wa Sudi
*Alinyanyaswa na mume wake.
*Ni mvumilivu katika matatizo.
*Ni mlezi bora wa familia.
*Anafaa kuigwa na jamii.
3. Bi Tatu
*Ni mpenda starehe.
*Hapendi kazi ambazo hazina mshahara.
*Anambembeleza mume wake kwa kuogopa kuachwa.
*Hafai kuigwa na jamii.
4. Bi Nne
*Ni mtu asiyependa maendeleo ya wenzake.
*Ana wivu, mbinafsi, mfitini na ana chuki binafsi.
*Hafai kuigwa na jamii.
5. Bi Tano
*Ni mke wa Maganga.
*Ana hasoira sana.
*Hakumpenda Bi Sita.
6. Bi Sita
*Alikuwa kahaba na alikuwa anatembea na waume za watu.
*Ni mkorofi na hakupenda ushirikiano.
*Hafai kuigwa.
7. Bi Saba
*Alifiwa na mume wake.
*Ni mlezi swa watoto.
*Ni kiumbe duni kwani shemeji zake walimnyang’anya
mali zake zote na hata watoto baada ya mume wake kufa.
8. Bi Nane
*Alipenda ushirikiano na swenzake.
*Alikuwa na elimuya kutosha.
*Alipenda kuelimisha wenzakekatika shughuli za
maendeleo.
*Hakuwa na chuki na mtu.
*Anafaa kuigwa.
9. Chizi
*Nmpenda demokrasia.
*Alipiga vita uoga.
*Ni mfichua maovu yaliyoko katika jamii
*Anaonesha wazi matatizo yanayosababisha
wanawakekushindwa kujikomboa.
*Anafaa kuigwa na jamii.
10. Mwenyekiti
*Ni mtu mwenye uongozi mbaya
*Anapenda kusiliza majungu na fitina.
*Anawachukia wanawake wasomi.
*Hafai kuigwa na jamii
.
MANDHARI
Mandhari ya tamthiliya hii ni ya kubuni. Yanasawiri
maisha ya vijijini na kiasi maisha ya mjini, kwani tunaona mwandishi ameonesha
mandhari ya vilabuni, uwanjani na nyumbani. Mandhari yaliyooneshwa yanaoana
sana nan chi za Kiafrikaa vile Tanzania, kwani unyanyasaji na ugandamizwaji wa
wanawake wa Kitanzania ni sawa kabisa na wale wa Patata.
JINA LA KITABU
Jina la kitabu Nguzo Mama linasadifu yale yaliyomo
ndani ya kitabu hiki. Kitaswira “Nguzo Mama” ni umoja wa wanawake Tanzania
(U.W.T) ambao uliundwa kwa lengo la kuwatetea, kuwalinda na kuwapa haki na
maendeleo wanawake sawa na wanaume. Tamthiliya hii inaonesha harakati za
wanawake wa Patata wakiwemo wakulima, wasomi, waalimu, makahaba na wanaungana
kuimarisha umoja na maendeleo yao. Wanafungua miradi mbalimbali kama vile
kushona, kupika pombe, pamoja na tofauti zilizopo kati yao kama vile uzembe,
majungu, fitina na kutoelewana.
KUFAULU NA KUTOFAULU KWA
MWANDISHI
KUFAULU
Kimaudhui mwandishi Penina Muhando amefaulu kwa kiwango cha juu
katika maudhui yaliyomo ndani ya mchezo huu, kwani amefaulu kutueleza matatizo
yaliyowapata wanawake wengi wa Kiafrika hususani  Tanzania.
Kifani, mwandishi ametumia lugha rahisi inayoeleweka, lugha
ya kishairi inayofurahisha pia na nyimbo zinazoburudisha. Hivyo kufanya mchezo
usichoshe.
KUTOFAULU
Kimaudhui, Penina Muhando ameshindwa kutueleza hatma ya wanawake
wa Patata na jamii nzima baada ya kushindwa kuinua nguzo mama.
Kifani, matumizi ya lugha ya matusi ni udhaifu wa mwandishi,
kwani matusi ni lugha isiyotakiwa katika jamii.
Share:

UHAKIKI WA TAMTHILIYA YA MORANI YA EMMANUEL MBOGO (Hassan Lemunje)

TAMTHILIYA: MORANI
MWANDISHI : E. MBOGO
WACHAPISHAJI : DUP
MWAKA : 1993
 Uhakiki wa Tamthiliya ya Morani| Kidato cha Tano na Sita ~ Mwalimu ...
UTANGULIZI
Morani ni tamthiliya inayoelezea  juu ya matatizo yaliyoikumba nchi yetu mwaka 1980 na kusababisha hali ngumu ya uchumi kwa tabaka la chini.Matatizo haya ni kama uhujumu uchumi, wizi wa mali ya umma, ulanguzi, rushwa na kukosekana kwa haki, unafiki wa viongozi wetu, matabaka,n.k.Mwandishi wa tamthiliya hii, E.Mbogo anaonesha kuwa, kukithiri huko kunakwamisha maendeleo hapa nchini.
 
FANI
MUUNDO
Mwandishi ametumia muundo wa moja kwa moja.Mchezo unaanza kuonesha kifo cha Dongo na utata uliojitokeza kwa wananchi juu ya kifo chake,Mchezo unaendelea kwa kueleza vita dhidi ya wahujumu uchumi na matokeo yake.Mchezo umegawanyika katika sehemu nne.
MTINDO
Msanii ametumia dayolojia ilivyo kawaida kwa tamthiliya – maelezo ya majibizano baina ya wahusika. Pia msanii ametumia nafsi zote tatu (yaani I, II, III)
Pia msanii ametumia nyimbo katika mchezo huu (uk 42).
MATUMIZI YA LUGHA
Lugha aliyotumia msanii ni ya kawaida inaeleweka na imejaa misemo,methali, tamathali za semi na mbinu nyingine za kisanaa.
MISEMO / NAHAU
v Ndumi la kuwili (uk 13)
v Anatuchomea utambi ( uk 15).
v Paka shume (uk 17).
v Kuwapaka watu matope (uk 29).
v Umeota meno jana (uk 8).
METHALI
v Penye nia pana njia na subira yavuta heri (uk 4)
v Siri ya kaburi aijua maiti na siri ya maiti aijua kaburi
v Fimbo ya mbali haiuwi nyoka (uk  23)
v Mfuga punda fadhila hukujambia  mashuzi (uk 23)
v Mwosha huoshwa (uk 24)
v Bandu bandu unataka kumaliza gogo? (uk 31)
v Usimsifu sana lasivyo tembo atalitia maji (uk 23)
v Mwenzako akinyolewa wewe tia maji (uk 23)
TAMATHALI ZA SEMI
TASHIBIHA
v Kesho tutawasambaza kama punje za mtama.
v Nungunungu na Mlemeta ni kama kupe na mkia wa ng’ombe.
v Watu wengi kama sisimizi (uk 39).
v Hii kampeni mmevaa tu kama koti la kutungua (uk 29).
TASHIHISI
v Jicho kali la hakimu lilimtambaa Kabwela Yule toka vidoleni hadi utosini.
v Jua lilipo tabasamu na kutandaza mbawa zake.
TAFSIDA
v Nikakumbatie blanketi mwenyewe? (uk 27)
v Tutaenda umana au wasiwasi? (uk 27).
MBINU NYINGINE ZA KISANAA
TANAKALI SAUTI
v Uuuuu!Uuuuuu!Dongo! Dongo jamaa.............(uk 1)
v  
TAKRIRI
v Mpumbavu mimi? Mimi  mpumbavu? (UK 26).
v Nimekosa nimekosa niseme hivi niseme (uk 22).
v Mnachuja, mnachuja mnachuja hadi lini? Mlemeta.
MDOKEZO
v Hallo bado tunaendelea na kazi .......mambo magumu mzee.....lakini nadhani tutayamudu......yaa saa ngapi.....sawa (uk 15)
v Lakini mzee.........(uk 18).
PICHA /TASWIRA
Msanii pia katumia lugha ya picha (uk 2), kuna picha ya mizuka inayolima shamba la tajiri – hiyo huwakilisha tabaka la wanyonge,watu wanaofanya kazi kubwa kwa kuwatajirisha matajiri wakati wao wenyewe wananyonywa.
Pili,kuna nguzo ya uswezi hii inaashiria mali za azimio la Arusha.Dongo anaashiria wanamapinduzi wanaotaka kuleta mabadiliko ya kisiasa, kiuchumi na utamaduni.Mti uliokuwa karibu na ofisi pamoja na wachawi hizi zote mbili huashiria wahujumu uchumi wetu.
Morani inaashiria vijana wanaotakiwa kuungana ili kuleta mabadiliko katika jamii.
WAHUSIKA
1.   DONGO
v Huyu ni mhusika mkuu wa tamthiliya hii anayepambana na hujuma ili kuwaendeleza na kuwasaidia wanyonge.
v Dongo alikuwa mstari wa mbele katika kupiga vita hujuma akisaidiwa na  Mapoto, Jalia, Malongo, Hadikwa. Dongo ni mfano wa viongozi wanamapinduzi anayefaa kuigwa na jamii.
2.   JALIA
v Ni mhusika mwanamke aliyejitoa mhanga kuongoza kampeni ya kutokomeza hujuma.
v Jalia aliongoza askari kumkamata Nungunungu bila woga.
v Pia katika maandalizi ya maandamano  Jalia alishirikiana na Mapoto, Malongo na Hadikwa katika kufanikisha maandamano hayo.
v Vilevile  alimpiga Yusufu na Nungunungu bila woga wala wasiwasi. Hivyo Jalia ni mwanamke anayefaa kuigwa na jamii kutokana na matendo yake.
3.   MAPOTO NA MALONGO
Hawa ni wahusika wadogo wa tamthiliya hii.
v Hawa wako pia mstari wa mbele kupiga vita rushwa, ukoloni, ubepari na hujuma
v Walishitikiana bega kwa bega na Jalia katika vita hiyo.
v  Ni mfano mzuri wa kuigwa na watu katika jamii yetu.
4.   NUNGUNUNGU
v Huyu anawakilisha wahujumu uchumi.
v Alikuwa anavusha kahawa na karafuu nchi za nje kwa magendo.
v  Ana hoteli Marekani na akaunti Uswisi.
v Ni mfano wa watu wanaolikosesha taifa letu fedha za kigeni kwa kufanya magendo yao, na ni mfano wa mtu mbaya asiyehitajika kuigwa na yeyote.
5.   YUSUFU NA MLEMETA
v Hawa ni viongozi wanafiki walioko mstari wa mbele katika kukwamisha shughuli zote za maendeleo.
v  Wanashirikiana na Nungunungu kuihujumu nchi yetu.
v Wakati wa kampeni za kutokomeza hujuma, walileta wahujumu mfano Nungunungu,hivyo hawafai kuigwa na jamii.
Ø Wahusika wengine ni Mzee, Aisha, Dala Bongi, Okashi n.k.
MANDHARI
Mandhari yake ni ya Kitanzania kutokana na matukio yanayoelezwa katika tamthiliya hii, yalijitokeza wazi katika jamii yetu ya Kitanzania.Matukio haya ni kama vile hali ngumu ya maisha,hujuma na vita dhidi yake.Matukio haya  ndiyo yaliyotawala  Tanzania kuanzia miaka ya 1980 na kuendelea.Vile vile  kuna mandhari ya nyumbani, ofisini, porini, baa, kumbi za tarehe, mitaani, hospitalini, n.k.
JINA LA KITABU
Kwa ujumla  jina la kitabulinasadifu yale yaliyomo ndani ya kitabu,msanii anatoa wito kwa vijana – Morani ili waweze kuungana na umma katika kupiga vita hujuma nchini.
KUFAULU KWA MWANDISHI
Mwandishi amefaulu kwa  kiasi kikubwa kwa kuionesha jamiiyetu matatizo yanayoikabili kama vile umaskini, hujuma, hali ngumu ya maisha,matabaka, na unafiki wa viongozi wetu na ametoa wito kwa vijana kushirikiana katika kupiga vita matatizo hayo.
Pia msanii amefaulu katika kuwachora wahusika wake wanamapinduzi. Kwa upande mwingine msanii amefanikiwa katika kuoanisha jina la kitabu na yaliyomo. Morani ni vijana wa Kimasai wenye jukumu la kulinda jamii yao. Katika kitabu hiki msanii anatoa wito kwa morani(vijana) wote kupiga vita hujuma hapa nchini.
KUTOFAULU

Msanii ametumia taswira nyingi mno si rahisi kwa mtu wa elimu ya chini kupata maana zake na hivyo hushindwa kupata ujumbe uliokusudiwa na mwandishi.
Share:

CLIC THE IMAGE SUBSCRIBE NOW

CLIC THE IMAGE SUBSCRIBE NOW
Bofya Picha Hiyo Hapo Juu Kisha Subscribe Channel Yetu ya Online Class Utapata Offer ya Kutumiwa Vitabu vyaasomo Yote Buree Kupitia Whatsap Yako

FUNDISHWA SASA NA TEACHER HASSAN LEMUNJE KWA NJIA YA MTANDAO KWA GHARAMA NAFUU.

FUNDISHWA SASA NA TEACHER HASSAN LEMUNJE KWA NJIA YA MTANDAO KWA GHARAMA NAFUU.
Popote ulipo bofya hapa uanze kufundishwa na Teacher Hassan Lemunje. Utatumiwa notes, voice notes za maelekezo kwa lugha nyepesi, pamoja na huduma ya solving ya mitihani yote ya Necta pamoja na Mock Regions sambamba na mbinu mbalimbali za kujibu na kufaulu mitihani Yako. Huduma hii ni kwa wanafunzi wa Level zote wenye kutumia WhatsApp. Piga Sasa uweze kuunganishwa (0622548220/076910272).

BLOGS AND GRAPHICS DESIGN; CONTACT US

Search This Blog

About Me

My photo
DAR ES SALAAM, MAPINGA BAGAMOYO, Tanzania
HASSAN AMONI LEMUNJE born in 31 August,1998. He is Professional Teacher as he teach various schools in Tanzania includes Mlali Sec school, Hijra Seminary, Jamhuri Sec school and currently at Baobab Sec school, an author, public speaker, Translator, Interpreter, and editor of various books, dissertations, term papers, research proposals, and articles.��His life purpose: To use my God-given talents to inspire, empower and become a good role model by supporting others to develop their potentials to the fullest and leave the world a better place than I found it & Yupo hapa kwaajili ya kukuletea masuala yote ya kitaaluma Nchini Tanzania. Pia anapatikana FACEBOOK TWETER na INSTAGRAM(@TeacherHassanLemunje) Contact me +255622548220 +255769010272