📖 elimu 🌑haibadili 🌎 dunia 📚 elimu 🌔 hubadili 👬🏾 watu na 👨‍👧‍👧 watu 🌏hubadili DUNIA🗼

1.26M Followers

1.26M Followers
1.26M Followers

UGA WA ELIMU

📕📕KARIBU TUSOME SASA KATIKA MAWANDA MAPANA📕📕 📕Tunarahisisha Usomaji📕Soma Kisasa📕

UHAKIKI WA RIWAYA YA MFADHILI KIDATO CHA 5_6 BY HUSEIN ISSA TUWA


JINA LA KITABU: MFADHILI.


MWANDISHI: HUSSEIN TUWA

MCHAPISHAJI: MACMILLAN

MWAKA: 2007

Utangulizi kuhusu Riwaya
Mfadhili ni riwaya iliyoandikwa na Hussein Tuwa, ni riwaya inayoongelea juu ya penzi zito baina ya watu wawili, Gaddi Bullah na Dania Theobald na jinsi ambavyo penzi hilo linavyoingiliwa na mitihani,majaribu na misukosuko mikubwa na namna ambavyo kila mmoja anavyojaribu kukabiliana na hiyo misukosuko. Ni riwaya inayogusa moyo na isiyochosha kusomwa na wasomaji wa kila aina.
Mwandishi Hussein Tuwa pamoja na kuandika riwaya hii, pia ameandika riwaya nyingine inayoitwa, Mkimbizi.
Utangulizi kuhusu uhakiki wa riwaya hii
Tunapofanya uhakiki wa kazi za fasihi huwa tunachambua vipengele mbalimbali  vya fasihi, vipengele hivyo ambavyo huchambuliwa ni fani na maudhui, katika fani huwa tunajishughulisha na Vipengele kama, wahusika, mandhari, mtindo, muundo, matumizi ya lugha, jina la kitabu na jalada, wakati katika maudhui huwa tunashughulika na vipengele kama vile dhamira, migogoro, ujumbe, falsafa ya mwandishi, mtazamo wa mwandishi.

*JINA LA KITABU*
Tukianza na jina la kitabu, jina la kitabu ni Mfadhili, kwa mujibu wa Kamusi ya kiswahili Sanifu [1981] nenoMfadhili limefasiliwa kuwa ni, “Mtu anayemfanyia wema mkubwa mtu mwingine” Kwa maana hiyo basi, kwa kiasi kikubwa jina la kitabu linasadifu yale yanayozungumzwa katika riwaya hii. Kwa mfano tunaona baada ya Dania kuanza kuumwa na Daktari kuthibitisha kuwa ana tatizo la ini juhudi za kumtafuta mfadhili atakayejitolea ini lake lipandikizwe kwa Dania zinafanyika kama mwandishi anavyosema; “Hawakuwa na la kufanya zaidi ya kuanza kutangaza kwenye vyombo vya habari vya ndani na nje ya nchi kuomba wasamaria wema watakaopenda kujitolea sehemu ya ini kumfadhili mgonjwa…” [Uk. 134]
Baada ya Juhudi zote kufanyika za kumtafuta mfadhili kufanyika hatimaye Mwandishi anaonesha kupatikana kwa mfadhili huyo, Mwandishi analithibitisha hili anaposema; “Nina taarifa njema muhimu kwetu sote…hatimaye mfadhili amepatikana!” [Uk 137]
Mwandhishi anamuonesha Gaddi Bullah kuwa ndiye aliyejitolea ini kumfadhili Dania na hivyo kuokoa uhai wa Dania, kama mwandishi anavyothibitisha akimtumia muhusika Dokta Virani anapomwambia Dania; “Gaddi Bullah ndiye mfadhiri wako Dania…” [Uk 140]
Vilevile jina la kitabu linasadifu yale yanayozungumzwa katika riwaya kwa sababu tunamwona Dania baada ya kupona anakuwa akijiuliza kila mara ni nani mfadhili wake? swali ambalo limekuwa likiusumbua moyo wa Dania, kama mwandishi anavyosema; “Ila sasa akili yake ikawa inajiuliza swali moja kila siku. Mfadhili wake ni nani?” [Uk 139]
Pia swala la ufadhili linajitokeza kwa Jerry amabaye anapata ufadhili wa kwenda kusoma Marekani, kama Mwandhishi anavyosema; “…Alikuwa amepata ufadhili wa shirika moja la kimataifa ambalo huwa linapokea maombi mengi sana ya ufadhili kuliko uwezo uliopo…” [Uk 83]
Pamoja na hayo kuna ufadhili mwingine unaofanywa na Dokta Virani kwa Bi. Hanuna, baada ya Bi. Hanuna kukamatwa na polisi na kuwekwa rumande ni Dokta Virani ndiye anayemfadhili kwa kumtoa kwa dhamana kama mwandhishi anavyosema; “Dokta Virani alipopata taarifa alihangaika huku na huko kumpatia dhamana, lakini ilishindikana.” Mwandishi anaendelea kusema; “Siku iliyofuata, Dokta Vilani alifanikiwa kumtoa kwa dhamana.” [Uk 127]
Ufadhili unaofanywa na Mama Mlole kwa Dania na Gaddi Bullah, licha ya kuwa Dania na Gaddi Bullah kuwa na matatizo ambayo yangeweza kuwafukuzisha kazi, Mama Mlole anafanya juhudi kubwa kushawishi uongozi wa kampuni ili waweze kuendelea na kazi kama mwandishi anavyosema akimtumia muhusika Mama Mlole anaposema; “Ndio…na kwa hatua aliyofikia, ilibidi aachishwe kazi, lakini kwa kumsaidia, nikiwa kama Afisa Utumishi wa kampuni, nilipendekeza apewe likizo….nilifanya kazi ya ziada kuushawishi uongo wa kampuni juu ya hili, jinsi nilivyofanya kazi ya ziada kulishawishi lile jopo la wakaguzi kule Arusha kukupa wewe nafasi nyingine…badala ya kukufaukuza kazi…”   [Uk 88]
Hivyo basi kwa ushahidi huo tunaweza kusema jina la kitabu linasadifu yale yote yanayozungumzwa katika riwaya hii.

BOFYA HAPA KUONA UHAKIKIZAIDI WA RIWAYA YA MFADHILI NA KUPAKUA PDF
Share:

CLIC THE IMAGE SUBSCRIBE NOW

CLIC THE IMAGE SUBSCRIBE NOW
Bofya Picha Hiyo Hapo Juu Kisha Subscribe Channel Yetu ya Online Class Utapata Offer ya Kutumiwa Vitabu vyaasomo Yote Buree Kupitia Whatsap Yako

FUNDISHWA SASA NA TEACHER HASSAN LEMUNJE KWA NJIA YA MTANDAO KWA GHARAMA NAFUU.

FUNDISHWA SASA NA TEACHER HASSAN LEMUNJE KWA NJIA YA MTANDAO KWA GHARAMA NAFUU.
Popote ulipo bofya hapa uanze kufundishwa na Teacher Hassan Lemunje. Utatumiwa notes, voice notes za maelekezo kwa lugha nyepesi, pamoja na huduma ya solving ya mitihani yote ya Necta pamoja na Mock Regions sambamba na mbinu mbalimbali za kujibu na kufaulu mitihani Yako. Huduma hii ni kwa wanafunzi wa Level zote wenye kutumia WhatsApp. Piga Sasa uweze kuunganishwa (0622548220/076910272).

BLOGS AND GRAPHICS DESIGN; CONTACT US

Search This Blog

About Me

My photo
DAR ES SALAAM, MAPINGA BAGAMOYO, Tanzania
HASSAN AMONI LEMUNJE born in 31 August,1998. He is Professional Teacher as he teach various schools in Tanzania includes Mlali Sec school, Hijra Seminary, Jamhuri Sec school and currently at Baobab Sec school, an author, public speaker, Translator, Interpreter, and editor of various books, dissertations, term papers, research proposals, and articles.��His life purpose: To use my God-given talents to inspire, empower and become a good role model by supporting others to develop their potentials to the fullest and leave the world a better place than I found it & Yupo hapa kwaajili ya kukuletea masuala yote ya kitaaluma Nchini Tanzania. Pia anapatikana FACEBOOK TWETER na INSTAGRAM(@TeacherHassanLemunje) Contact me +255622548220 +255769010272