📖 elimu 🌑haibadili 🌎 dunia 📚 elimu 🌔 hubadili 👬🏾 watu na 👨‍👧‍👧 watu 🌏hubadili DUNIA🗼

1.26M Followers

1.26M Followers
1.26M Followers

UGA WA ELIMU

📕📕KARIBU TUSOME SASA KATIKA MAWANDA MAPANA📕📕 📕Tunarahisisha Usomaji📕Soma Kisasa📕

UHAKIKI WA DIWANI YA MALENGA WAPYA BY TAKILUKI (Hassan Lemunje)

HAKIKI WA DIWANI YA MALENGA WAPYA

WAANDISHI: TAKILUKI

WACHAPISHAJI: O.U.P

 MWAKA : 1997

UTANGULIZI
Malenga Wapya | Text Book Centre

MALENGA WAPYA ni diwani yenye mkusanyiko wa mashairi yapatayo thelathini na saba (37) yaliyoandikwa na washairi wapya(malenga wapya). Washairi hawa ni wanafunzi wa Taasisi ya Kiswahili na Lugha za Kigeni huko Zanzibar.

Katika diwani hii ,washairi wamejadili masuala mbalimbali yanayotokea katika jamii. Baadhi yake ni masuala ya kisiasa, kiuchumi, kijamii n.k.Washairi hawa wamejadili masuala ya msingi katika kujenga jamii mpya na kama yatazingatiwa mabadiliko chanya yatatokea kwenye jamii.

MATUMIZI YA LUGHA

Katika ushairi kipengele cha lugha huhisisha taswira, tamathali za semi, methali, nahau,misemo na mkato wa maneno.

Taswira (picha/jazanda) hiki ni kipengele cha lugha ambacho huchora au huwasilisha wazo kwa kutumia picha au taswira mbalimbali,mfano katika shairi la SAMAKI MTUNGONI kuna taswira ya samaki ikiwakilisha watu wa tabaka la chini (watawaliwa), taswira ya mvuvi ni watu wa tabaka la juu (viongozi) na taswira ya mtungo ni sheria,kanuni au taratibu zinazotumiwa kuwabana watu wa tabaka la chini.

  Ø Njiwa  mpenzi shairi la NIPATE WAPI MWINGINE?

  Ø Punda- tabaka linalokandamizwa (shairi la PUNDA)

  Ø Ua – mwanamke/ msichana (shairi la UA)

METHALI

Kuna methali mbalimbali zimetumiwa katika diwani hii; mfano

  Ø Subira yavuta heri (shairi la SIHARAKIE MAISHA)

  Ø Aisifie mvua kaloa mwilini mwake (shairi la SISUMBUKIE KICHAA)

  Ø Fahari – wapiganapo nyasi ndizo huonewa (SOKOMOKO BAHARINI)

MISEMO

  Ø Siharakie maisha (SIHARIKIE MAISHA)

  Ø Sisumbukie kichaa (SISUMBUKIE KICHAA)

  Ø Sokomoko baharini (SOKOMOKO BAHARINI)

TAMATHALI ZA SEMI

TASHIBIHA

  Ø Ubaguzi umezama kama nguzo (shairi la TUNZO)

  Ø Maisha ni kama njia (shairi la MAISHA NI KAMA NJIA)

  Ø Yametolewa na kombe mithili ya gome la mti (shairi la BAHARI)

TASHIHISI

  Ø Samaki wakasirika (shairi la SAMAKI MTUNGONI)

  Ø Njaa imetuvamia (shairi la ADUI)

  Ø Ua limejituliza (shairi la UA)

  Ø Ulimi ninakuasa (shairi la ULIMI)

TASHITITI

  Ø Katika shairi la MWABAJA MWASEMA NINI?

  Ø Nasikia mwatunga,mwatungani washairi

TANAKALI SAUTI

  Ø Parakacha mlio wa majani makvu (shairi la KWA NINI?)

  Ø Kokoriko – shairi la MKULIMA

TAKRIRI

  Ø Kuna takriri kituo cha mfano shairi la KWA NINI?

MKATO WA MANENO



  Ø Kuna maneno yamekatwa ili kuepuka urari wa vina na mizani mfano “anong’ona (shairi la KWA NINI?).

Bofya Hapa Kuendelea
Share:

UHAKIKI WA DIWANI YA WASAKATONGE NA MUHAMED SEIF KHATIBU

Academic : Wasakatonge
JINA LA KITABU; WASAKATONGE
MWANDISHI; MUHAMMED SEIF KHATIB
MCHAPISHAJI; OXFORD UNIVERSITY PRESS
MWAKA; 2003

UTANGULIZI
Wasakatonge ni diwani inayozungumzia hali ngumu ya maisha. Matatizo anayoyataja mshairi ni magumu kutibika mfano wa saratani, hata hivyo wananchi wakiungana na kupambana pamoja jamii mpya yenye misingi ya usawa itapatikana.
Diwani ya Wasakatonge ni miongoni mwa diwani za hivi karibuni zinazotanabaisha matatizo mbalimbali yanayoikumba jamii katika maisha yake ya kila siku. Matatizo hayo yanaonekana kuwa kama saratani isiyo na tiba. Hata hivyo, msanii ana matumaini kwamba, iwapo wananchi wa kawaida wataungana na kuamua kupambana, ni dhahiri kwamba matatizo hayo yatatoweka kabisa. Miongoni mwa matatizo hayo yataoneshwa kwenye kipengele cha maudhui huku yakishadidiwa na fani.
MAUDHUI: ni jumla ya mambo muhimu yanayoelezwa katika kazi ya kifasihi. Maudhui yanajengwa na vipengele vidogovidogo vifuatavyo; dhamira, ujumbe, mgogoro, mtazamo na falsafa.
DHAMIRA: ni jumla ya maana anayovumbua mwandishi aandikapo kazi yake na jumla ya maana anayoipata msomaji pindi anapoisoma kazi fulani ya kifasihi. Kifasihi kuna aina mbili za dhamira yaani dhamira kuu na dhamira ndogondogo. Dhamira kuu ni lile wazo kuu la mwandishi katika kazi, wakati dhamira ndogondogo ni zile dhamira zinazojitokeza ili kuipa nguvu dhamira kuu. Dhamira zilizojitokeza katika diwani hii ni kama ifuatavyo:
UONGOZI MBAYA: ni aina ya uongozi ambao haujali maslahi ya wananchi na taifa kwa ujumla. Ni uongozi unaotumia mabavu na unaojali maslahi binafsi, yaani haufuati misingi ya utawala wa sharia. Katika diwani hii msanii anaonesha kuwa nchi nyingi duniani hasa zile za kiafrika zinakabiliwa na tatizo la uongozi mbaya. Viongozi walio wengi ni madikteta ambao hawataki kuachia madaraka wala kuwapa watawaliwa uhuru wa kuzungumza.
Hali hii tunaopata katika shairi la “MADIKTETA” (uk.21) ambapo msanii anasema kuwa harakati za kusaka uhuru au demokrasia kwa njia ya mtu haijawahi kuzaa matunda yanayotarajiwa. Harakati hizi zimekuwa zikizalisha viongozi “Miungu watu” au marais walio madikteta, kama ilivyokuwa kwa Mabutu Seseko-huko Zaire (kwa sasa DRC), Bokosa-huko Afrika ya Kati na Idd Amini-huko Uganda. Madikteta hawa wamekuwa na kila aina ya uovu ikiwa ni pamoja na kukumbatia ukabila, udini na uvamizi kwa nchi nyingine. Haya tunayapata katika shairi la “SADDAM HUSSEIN” (uk.26:4) anasema;
4.    “Nakuafiki, Saddam, si kwa uvamizi wako,Na ujue kwamba,
                                                  Huo si uasi
                                      Kwa wakubwa mila, 
                                Saddam, yamesha tendeka sana!”
Viongozi wa aina hii huwanyima wananchi wao uhuru wa kusema ikiwa ni pamoja na ule wa kujiamulia mambo yao wenyewe kama katika shairi la “MARUFUKU” namba 45 (uk.36)
                               “Sitakiki uone,
Ingawa una macho,
      Sitaki useme,
Ingawa una mdomo,
                   Sitaki usikie,
Ingawa una masikio,
      Sitaki ufikiri,
Ingawa una akili,
                   Sababu utazinduka,
Utakomboka,
                   Uwe mtu,
Hilo sitaki,
                    Marufuku.”     
Viongzozi wabovu (madikteta) ni wapenda dhuluma na manyanyaso. Huwadhulumu na kuwanyanyasa raia wao na raia wa nchi nyingine kama inavyojidhihirisha katika mashairi ya “KOSA” (uk.3), na “FAHARI LA DUNIA” (uk.45). Katika shairi la “KOSA”, tunaona kuwa unyanyasaji wa wananchi wa kawaida hutokea pale ambapo wanapokuwa wanadai haki zao. Mshairi anasema:
3. “Kosa letu kubwa,
     Kudai haki?
    Yetu miliki?
   Mna hamaki,
       Na huku mnatukashifu!”
Katika shairi la “FAHARI LA DUNIA” (uk.45) tunaambiwa kuwa kuna kiongozi mwenye nguvu (Marekani) ambaye mchana kutwa usiku kuchwa linanyanyasa nchi nyingi bila sababu za msingi. Msanii anasema:
 5.     “Fahari la Dunia,
    Kwa kiburi, linatesa,
       Lajigamba,
      Linatamba,
                Kuwa mwamba,
               Linaoneya.”
 Viongozi wabovu siku zote ni wanyonyaji na hushirikiana na watu wengi wenye nguvu kubeba mirija ya unyonyaji na kuanza kuwanyonya raia wa kawaida. Hali hii hujitokeza sana katika nchi za Dunia ya tatu. Haya yote tunayapata katika mashairi ya “MVUJA JASHO” (uk.12-13), “MIAMBA” (uk.29-30), “MUMIANI” (uk.34) Katika shairi la “MVUJA JASHO” msanii anaonesha kuwa raia wa kawaida wanafanya kazi kubwa na ngumu sana lakini malipo yao hayalingani na jasho wanalolitoa. Katika shairi la “MIAMBA” tunaambiwa kuwa wanyonge hawana chao, jasho lao na wao wenyewe ni chakula cha wakubwa na watawala wao. Ubeti wa 4 wa shairi hili msanii anahoji juu ya suala hili kwa kutumia taswira ya wanyama:
4. “Wanyonge,
     Wamo shidani,
     Digidigi na nyani,
     Wamo makimbizoni,
     Fisi wafurahia,
                    Ni sharia za mbuga?”
Katika shairi la “MUMIANI” linaonesha waziwazi unyonyaji unaofanywa na viongozi au watu wa tabaka la juu dhidi ya tabaka la chini ambao wanaishi vijijini na mijini, waendao hospitalini na wapelekwao mahakamani. Katika ubeti wa 1 tunaambiwa kuwa:-
1.      “Mumiani,
Mijini,
Watembea kwa mato,
Kuzifanya kazi zao,
Kuzinyonya damu zetu,
Hawangoji,
   Tulale.”
Diwani hii inaendelea kuonesha kuwa viongozi wabovu ni wasaliti na wanafiki. Viongozi hawa wanakuwa wepesi kuwaomba wananchi ili kufanikisha jambo fulani. Lakini pindi jambo hilo linapofanikishwa tu viongozi hao huwaweka wananchi pembeni (huwasaliti wananchi). Miongoni mwa mashairi yanayoonesha usaliti na unafiki wa viongozi wa dini na wa kisiasa ni “SIKULIWA SIKUZAMA” (uk.22-23), “WASO DHAMBI” (uk.1), “UASI” (uk.8), “PEPO BILA KIFO” (uk.14), vilevile shairi la “NAHODHA” (uk.41) linaonesha kuwa kuna viongozi wengi wanaoshindwa kazi lakini hawataki kuachilia madaraka. Hata hivyo msanii anaonesha kuwa viongozi wa aina hii wanaweza kuondolewa madarakani iwapo tu wananchi wote wataungana na kuwapiga vita.

Share:

UHAKIKI WA TAMTHILIYA YA ORODHA BY STEVE REYNOLDS (Hassan Lemunje)

Uhakiki wa Tamthiliya ya Orodha ~ Mwalimu Makoba

UHAKIKI WA TAMTHILIYA YA ORODHA
Mtunzi: Steve
REYNOLDS
Mchapishaji : Macmillan
Chapaya
1;2006
UTANGULIZI
ORODHA ni
miongoni mwa tamthiliya ambazo zinaonyesha namna jamii hususani watoto na
vijana wanavyoangamia kutokana na UKIMWI.Vijana wengi wanaangamia kwa sababu ya
ukosefu wa elimu sahihi kuhusu UKIMWI hali hii yaweza kusababisha ongezeko la
waathirika,Binti mdogo furaha kwa kutokujua athari za UKIMWI anajiingiza kwenye
vitendo vya ulevi na uzinzi kama alivyoshauriwa na rafiki yake Marry na
kujikuta akipata UKIMWI mapema hivyo ni vyema asasi kama za dini zihusike
katika kutoa elimu hiyo

FANI
Mwandishi
amewagawa wahusika katika makundi mawili yaani wahusika wakuu na wahusika
wasaidizi
A.   WAHUSIKA WAKUU
·
Mhusika
mkuu katika tamthiliya hii ni Furaha,
·
Msichana
aliehitimu darasa la saba,
·
Furaha
alijihusisha katika mambo ya uzinzi akiwa na umri mdogo
·
Furaha
hakuwa mtiifu kwa wazazi wake kwani licha ya kukatazwa tabia ya utoro wa usiku
na ulevi hakuacha tabia hiyo bali aliendelea mpaka alipopata maambukizi ya VVU
·
Hakuwa
mwaminifu kwa mpenzi wake Salim,alikuwa muongo kwani alimdanganya Salim hana
mwanaume mwingine zaidi yake,
·
Alijihusisha
kimapenzi na watu waliomzidi umri ambao sawa na baba yake mfano bwana Ecko na Padri James
·
Alikuwa
na tama ya pesa na vitu ,alidanganyika kirahisi mfano Marry alimdanganya kuwa
mwema kwa akina bwana Ecko.
·
Si mwaminifu,
·
Muwazi,
·
Mwenye
upendo yuko mstari wa mbele kupambana naVVU/UKIMWI
B.   WAHUSIKA WASAIDIZI
Mama Furaha
·
Ni
mama mzazi wa Furaha
·
Ni
mchapakazi
·
Ni
mpole
·
Ni
mama mwenye upendo
·
Mkweli
·
Ni
muwazi
·
Ana
msimamo
·
Anafaa
kuigwa na jamii kwani ni mama aliyeejishughulisha  katika ulezi wa watoto na familia nzima
Baba Furaha
·
Ni
baba mzazi wa Furaha
·
Ni
mkali
·
Ana
upendo
·
Ana
lugha kali kwa wanae
Marry
·
Ni
msichana
·
Ni
rafiki yake Furaha
·
Ni
Malaya
·
Mlevi
·
Hafai
kuigwa na jamii
Bwana Ecko
·
Ni
mwanaume mtu mzima
·
Ni
mfanya biashara
·
Ni
mlevi
·
Hafai
kuigwa na jamii,sio mwadilifu katika ndoa yake,ni mwathirika wa UKIMWI
Bwana Juma
·
Ni
mwanaume mtu mzima
·
Ni
rafiki yake na bwana Ecko
·
Ni
mzinzi
·
Ni
mtu mwenye tama
·
Ana
lugha chafu hafai
·
Hafai
kuigwa na jamii
Kitunda
·
Ni
kijana wa mtaani
·
Ni
rafiki yake na Furaha
·
Ni
msanii
·
Sio
mwadilifu
·
Sio
muwazi
·
Sio
mkweli
·
Anaweza
kuwa mwathirika wa UKIMWI japokuwa alitumia kondomu baadhi ya siku alizokutana
na Furaha
MTINDO
Mwandishi wa
tamthiliya hii ametumia mitindo mbalimbali katika kazi yake mfano matumizi ya
majibizano (dayaloji)Mtindo huo huruhusu wahusika wake kuzungumza kwa
kujibizana mfano mazungumzo kati ya Furaha na Kitunda
Furaha:kuvuta
nini lako……..(anarudi nyuma)
Kitunda:Mezea
mtoto lazima ujifunze lugha za mitaani
MUUNDO
Mwandishi wa
tamthiliya hii ametumia mtindo wa onyesho ambao sehemu hizo zipo kwenye makundi
matatu ambayo yamejipambanua kutokana na matukio mfano sehemu 1-2 ni mazishi ya
Furaha ,sehemu ya 3-16 ni makuzi ya maisha ya Furaha kwa ujumla ikihusisha
kuugua na kifo chake ,sehemu ya 17-20 ni mwendelezo wa mazishi ya Furaha
ikiwemo mchakato wa kutafuta barua ya furaha (orodha)mchakato unaofanywa a
Bwana Ecko,Padri James na Salim na mwiso wa mazishi ulioamatana na kusomwa
barua ya orodha
MANDHARI
Mwandishi
ametumia mandhari ya kijijini.Hii inawakilisha vijiji mbalimbali hapa Tanzania
na Bara la Afrika kwa ujumla ,mahala ambapo elimu kuhusu UKIMWI haijaeleweka
vema au hakuna kabisa pia huduma za afya kama hospitali hakuna kabisa
MATUMIZI YA LUGHA
Lugha
iliyotumika ni ya kawaida inaeleweka na inazingatia maadili ya kitanzania na
kueleweka vema kwa walengwa na kwa kiasi fulani tamathali za semi na mbinu
nyingine za kisanaa
Misemo/Nahau
Misemo
iliyotumika kwenye tamthiliya hii ni kama ifuatavyo ,
  v
“Shuga
dadi”mwandishi akiwa anamaanisha wanaume wenye umri mkubwa wanaopenda
kutembea na wasichana wadogo umri sawa na binti zao
  v
“mshamba
“mtu ambae hajui mambo ya mjini au mambo ya kileo
  v
“furaha
anavuna mbegu ya kifo aliyoipanda”kuvuna ni msemo                   unaomaanisha kupata
kitu kutokana na matenyo au maandalizi ,msemo huu ni sawa na “utavuna
ulichopanda”
  Ø
MISIMU
Mwandishi
ameweza kutumia lugha ya misimu ili kuweza kumtambulisha muhusika ,misimu
iliyotumika ni ile ya mitaani au ya vijana kutoka kijiweni ,lugha hii tunaweza
kuona ikitumika katika mazungumzo kati ya Kitunda na Furaha mfano
mshikaji,mchizi ,bomba ,poa majani,nitakulinda ,mwanangu ,kuvinjari haya ni
baadhi ya maneno yanayotumika mitaani hususani maneno haya hutumika na vijana
wa kijiweni katika mji
Maana ya
maneno hayo
Mshikaji-rafiki/jamaa
Bomba
mchizi –sawa rafiki/ndugu
Poa-vizuri
/sawa
Ganja,majani-bangi
Nitakilinda-nitakusaidia
Mwanangu-mtu
wa karibu/rafiki yangu
Kuvinjari-kuzunguka/kutalii
TAMATHALI ZA SEMI
Mfano ….yeye
ni kama punda wa kijiji tamathalii hii ilitumiwa kumfananisha Furaha na punda
wa kijiji ambae kila mwaname anampenda ,ilitokana na tabia ya Furaha kuwa
uhusiano wa kimapenzi na wanaume mbalimbali
Pia Kitunda
anafananisha jiji la Dar-es salam sawa na jiji la New york anasema….kisura
sawa na jiji la New york
Pia mwandishi
anapoonyesha namna vipande vya karatasi vilipoanguka baada ya barua ya orodha
kuchanwa na Salim anasema…..vipande vikaanguka kama theluji
  Ø
SITIARI
Tamthiliya hii imetumiwa
na baba Furaha anapofananisha watoto wake ma mbu wanyonyao damu wasioweza
kujitegemea anasema “nyie mbu wadogo”
  Ø
KIJEMBE
Mwandishi
ametumia kejeli kati ya Marry na bwana Juma anasema
Marry:nielezewewe
ni mzee wa kutosha kuwa baba angu
  Ø
TAFSIDA
Pia mwandishi
ametumia tafsida ili kupunguza ukali wa maneno aliyoyatumia
Mfano :Bwana Ecko:Juma hebu mwangalie yule
msichana anavyotingisha kile alichopewa na mama yake
Bwana
Juma:kama ulivyofanya wewe mishikaki yangu midogo
Tamathali
hiyo(tafsida)imetumiwa badala ya kutaja sehemu zake za siri anazozizungumzia
  Ø
TASWIRA
Mwandisha pia
ametumia lugha ya picha(taswira)
Mfano,karibu nitakufa njaa hali nyie mbu wadogo
mnainyonya damu yangu yote,mbu ni taswira inayoonyesha hali ya utegemezi
JINA LA KITABU
Kitabu hiki
kinaitwa ORODHA (The list)neno lenye
maana la mfuatano au mfululizo wa vitabu au mambo.Kitabu hiki kinaonyesha
orodha zifuatazo
Mosi,Orodha
ambayo Furaha alibainisha mambo ambayo yalisababisha kifo chake.mfano;ngono zembe,ukosefu
wa elimu,kukosekana kwa uaminifu,umasikini.
Pili,kuna
orodha ambayo ina mambo ambayo jamii inapazwa kujazingatia ili waepuke UKIMWI
ambayo ni ngono salama,uadilifu,uaminifu,elimu sahihi kuhusuVVU?UKIMWI

BOFYA HAPA KUENDELEA
Share:

UHAKIKI WA KILIO CHETU BY MEDICAL AID FOUNDATION (Hassan Lemunje)

Kilio Chetu – Mkuki na Nyota Publishers
JINA LA TAMTHILIYA: Kilio Chetu
MWANDISHI: MEDICAL  AID FOUNDATION
MCHAPISHAJI: TANZANIA PUBLISHING HOUSE (TPH) MWAKA 1995


Mwaka 2014
                                                          UTANGULIZI
Kilio Chetu ni tamthiliya inayojikita kuzungumzia umuhimu wa elimu ya jinsia na ukimwi kwa vijana, Tamthiliya hii inaonesha namna ukosefu wa elimu ya jinsia na ukimwi kwa jamii hususani vijana inavyochangia mimba za utotoni au mimba zisizotarajiwa na maambukizi ya virusi vya ukimwi kwa vijana.
Katika tamthiliya hii, mwandishi anaonesha namna ambavyo jamii ikiangaika kujielimisha kuhusu elimu hii ya jinsia na ukimwa na kuwaacha vijana wakiangamia kwa kukosa elimu hiyo, hali hii inaifanya jamii kugawanyika, wapo wanaoona kuwa suluhisho la janga hili la Ukimwi, ni jamii nzima wakiwemo na vijana kupewa elimu hii lakini wapo wazazi wanaopinga wakiamini vijana umri wao wakupewa elimu hii haujafika bado. Je ni nini hatima ya vijana hawa? Basi tafuta kitabu hiki cha Kilio chetu kisome utajifunza mambo mengi sana ni kitabu kinachotakiwa kusomwa na watu wa rika lolote.
WAHUSIKA
Katika kazi ya fasihi wahusika wanaweza kuwa watu, wanyama au vitu, na wahusika ndiyo wanaobeba dhamira za msanii, na katika kazi ya fasihi wahusika tunawagawa katika makundi mawili, wahusika wakuu na wahusika wasaidizi/ wahusika wadogowdogo


(a)  Wahusika Wakuu
Katika tamthiliya hii, ina wahusika wakuu wawili, ambao ni Suzi na Joti.
1.     SUZI
ü Ni binti anayesoma shule ya msingi
ü Ni binti asiyekuwa na elimu ya jinsia na ukimwi, Mama yake anashindwa kumpa elimu hiyo akiamini kuwa umri wa Suzi haujafikia kupewa elimu hiyo.
ü  Anajiingiza katika mapenzi akiwa mdogo.
ü Anakuwa na mahusiano ya kingono na mwanafunzi mwenzake anayeitwa Joti.
ü Ni binti wa pekee wa Mama Suzi.
ü Anapata mimba akiwa mwanafunzi na anafikiria kuiotoa mimba hiyo.

2.     JOTI
ü Ni kijana wa kiume anayesoma shule ya msingi.
ü Ni kijana asiyekuwa na elimu ya jinsia na ukimwi, baba yake anashindwa kumpa elimu hiyo akiamini kuwa umri wa joti haujafikia kupewa elimu hiyo.
ü Anajiingiza katika mahusiano ya kingono akiwa mdogo huku akiwa mwanafunzi.
ü Anajihusisha na mahusiano ya kingono na wasichana wengi, akiwemo Suzi, Chausiku, Gelda n.k.
ü Ni mvulana mlaghai, anawalaghai wasichana ili tu kutimiza haja zake za kingono.
ü Anaambukizwa virusi vya ukimwi
ü Anafariki kwa ugonjwa wa ukimwi.

(b) Wahusika wadogo wadogo
1.     MAMA SUZI
ü Huyu ni mama yake Suzi
ü Anamlea Suzi bila baba
ü Anajishughulisha na biashara ndogondogo kama vile kuuza vitumbua ili kujipatia kipato.
ü Anaamini kuwa mtoto mdogo hawezi kuambukizwa virusi vya ukimwi.
ü Anakumbatia mila na desturi zililozipitwa na wakati zinazokataza watoto/vijana kupewa elimu ya jinsia na ukimwi.
ü Anakataa katakata mtoto wake, Suzi kupewa elimu ya jinsia na ukimwi akiamini kuwa umri wake ni mdogo, na kufanya hivyo ni sawa na kumfundisha umalaya.
ü Anamwadhibu mtoto wake (Suzi) baada ya kukuta vidonge vya kuzuia mimba katika mfuko wa sketi yake.

2.     BABA JOTI
ü Ni baba yake na Joti.
ü Anaamini kuwa ukali wa mzazi na viboko ndiyo suluhisho la kuwazuia watoto kujiingiza katika mambo mabaya.
ü Anakataa katakata elimu ya jinsia na ukimwi kutolewa kwa watoto/vijana.
ü Anaangaika kuokoa uhai wa mtoto wake, Joti, kwa kutafuta tiba yake kila mahali.
ü Anampoteza mtoto wake(joti) baada ya kufariki kutokana na ukimwi.

3.     MAMA JOTI
ü Huyu ni mama yake Joti.
ü Mke wa Baba Joti
ü Rafiki yake Mama Suzi
ü Anahisi mume wake ana uhusiano wa kimapenzi na wanawake wengine, hali inayomlazimu kuwanunulia kanga zenye maandishi ya mafumbo ili kuwapasha wezi wake.
ü Yeye na mumu wake (Baba Joti) wanashindwa kumpa Joti elimu ya jinsia na ukimwi.
4.     BABA ANNA
ü Huyu ni baba yake Anna.
ü Anaamini kuwa elimu ya jinsia na ukimwi ni muhimu kwa vijana ili kuwanusuru na janga la ukimwi.
ü Kwa kushirikiana na mke wake wanafanikiwa kuwapa watoto wao elimu ya jinsia na ukimwi, elimu inayowasaidia kupambana na vishawishi.

5.     MAMA ANNA
ü Huyu ni mama yake Anna.
ü Ni mke wa Baba Anna
ü Kwa kushirikiana na mume wake wanafanikiwa kuwapa watoto wao elimu ya jinsia na ukimwi, elimu inayowasaidia kupambana na vishawishi.
6.     ANNA
ü Mtoto wa kike wa Baba Anna na Mama Anna
ü Ni mwanafunzi wa Shule ya msingi.
ü Amepewa elimu ya jinsia na ukimwi, elimu inayomsaidia kupambana na vishawishi vya kujiingiza katika mahusiano ya kimapenzi akiwa mdogo
ü Ana mkatalia Mwarami kuwa naye kimapenzi

7.     MJOMBA
ü Huyu ni kaka yake na Mama Suzi
ü Mjomba wake na Suzi
ü Anasisitiza elimu ya jinsia itolewe kwa vijana wote ili kuwanusuru na maambukizi ya virusi vya ukimwi na mimba zisizotarajiwa.
ü Anamshauri Baba Joti kutoangaika kwenda kwa waganga na kumaliza rasilimali zake kwa ajili ya kutafuta tiba ya UKIMWI kwa mtoto wake Joti  kwani ukimwi hauna dawa

8.     JIRANI
ü Huyu ni jirani yake na Baba Joti.
ü Anamshawishi Baba Joti kwenda kwa mganga wa kienyeji kutibiwa ukimwi.

9.     MWARAMI
ü Huyu ni rafiki yake Joti, Choggo na Jumbe
ü Ni mwanafunzi wa shule ya msingi
ü Hana elimu ya jinsia na Ukimwi anaamini ukimwi unawapata wakubwa tu
ü Wenzake wanamshawishi kujiingiza katika mahusiano ya kimapenzi na hata kumtishia asipofanya hivyo watamfukuza katika kundi lao la urafiki
ü Anashindwa kumshawishi Anna

10.                     CHOGGO
ü Huyu ni rafiki yake Joti, Mwarami na Choggo
ü Ni mwanafunzi wa shule ya msingi
ü Anajiingiza katika mahusiano ya kimapenzi akiwa mtoto mdogo tena mwanafunzi
ü Yeye na rafiki zake wana tabia ya kwenda katika vibanda vinavyoonesha video za ngono (sinema za X) kuangalia

11.                     JUMBE
ü Huyu ni rafiki yake Joti, Mwarami na Choggo
ü Ni mwanafunzi wa shule ya msingi
ü Anajiingiza katika mahusiano ya kimapenzi akiwa mtoto mdogo tena mwanafunzi
ü Yeye na rafiki zake wana tabia ya kwenda katika vibanda vinavyoonesha video za ngono (X) kuangalia

12.                     CHAUSIKU
ü Huyu ni mwanamke mtu mzima jirani na akina Joti.
ü Anajishughulisha na biashara ndogondogo hususani biashara ya vitumbua ili kujipatia kipato.
ü Anakuwa na mahusiano ya kimapenzi  na kijana mdogo tena mwanafunzi (Joti)
ü Ana mahusiano ya kimapenzi na Mpemba muuza duka.

13.                     FAUSTA
ü Huyu ni msichana anayesoma darasa  la tano
ü Anafariki kwa ukimwi

14.                     MPEMBA
ü Huyu ni mfanyabiashara wa duka
ü Anakuwa na mahusiano ya kimapenzi na Chausiku

Mfano wa maswali unayoweza kuulizwa sehemu hii
1.     Wahusika na hasa mhusika mkuu katika tamthiliya  ndiye anayeifikishia jamii ujumbe uliokusudiwa. Tumia tamthiliya mbili kutetea hoja yako.
2.     Chagua wahusika watatu wa kike kutoka kila tamthiliya kati ya tamthiliya mbili ulizosoma, kasha onesha kukubalika kwao kama kielelezo cha maisha katika jamii.
                             
DHAMIRA
Hili ni wazo kuu au mawazo mbalimbali yanayojitokeza katika kazi ya fasihi. Na katika tamthiliya hii kuna  dhamira kuu na dhamira ndogondogo ambazo zimejitokeza, kwa kuanza tunaanza na;

(a)  Dhamira Kuu
Dhamira kuu katika tamthiliya ni umuhimu wa elimu ya jinsia na ukimwi, mwandishi anaamini kuwa, ili jamii iweze kunusurika na matatizo yatokanayo na kujamiana kama vile mimba za utotoni (mimba zisizotarajiwa) magonjwa ya zinaa kama vile kasendwe, kisonono gono na ukimwi, sharti vijana wapewe elimu ya jinsia na ukimwi, mwandishi anathibitisha hili akimtumia muhusika Mjomba anaposema, “Upepo umebadilika sasa. Hawa vijana wetu wapewe elimu ya familia ikiwepo ya jinsia. Watoto waambiwe wazi juu ya mambo haya ya mapenzi na hatima yake.” Uk. 9

Vilevile, mwandishi anaonesha namna ambavyo vijana wanapukutika, wanaangamia na ukimwi kwa sababu ya kukosa elimu hii ya jinsia na ukimwi, hali hii inasababisha vijana kuwa gizani kabisa wanashindwa namna ya kujikinga na wengine hata kushindwa kutofautisha kati ya puto na kondomu , rejea ukurasa wa 13, Mwandishi akimtumia muhusika Mtambaji anaposema, “Kisiwa kizima kipo gizani. Watoto ndio kabisa. Wapo katika giza nene. Wanashindwa kutofautisha kati ya puto na kondomu.”

Si hivyo tu, mwandishi anaendelea kutuonesha kuwa, ukosefu wa elimu hii ya jinsia na ukimwi kwa vijana/watoto inawafanya watoto/vijana kujitenga na mapambano dhidi ya ukimwi kwakuwa wao wanaamini kuwa ugonjwa huu wa ukimwi ni wa wakubwa tu kwani watoto hawawezi kuambukizwa virusi vya UKIMWI kama mwandishi anavyosema akimtumia muhusika Mwarami anapomwabia Anna, “Ukimwi unawapata wakubwa, Anna.” Uk. 25

Si watoto tu, wapo hata wazazi, watu wazima ambao nao wanaamini kuwa watoto wadogo hawawezi kuambukizwa virusi vya ukimwi, kama anavyoamini Mama Suzi, rejea ukurasa wa 4, muhusika Mama Suzi anaposema, “...Lakini shoga, watu wanatafuta laana ya marehemu. Kitoto kama kile; kife kwa ukimwi! Ungeingilia kona gani?” {Uk.4}

Mwandishi anaendelea kutuonesha kuwa, hata mimba za utotoni, mimba zisizotarajiwa kwa vijana husababishwa na ukosefu wa elimu hii ya jinsia, kwa mfano mwandishi anamtumia muhusika Suzi ambaye anaamini kuwa, kwa kufanya ngono mara moja hakuwezi kusababisha mtu akapata mimba, hili tunaliona ukurasa wa 28, Suzi anapomwambia Anna, “Wala sina mimba, kwanza mimi nimefanya mara moja tu na joti.” {Uk.28}

Vilevile, mwandishi anaonesha kuwa, wapo watoto/vijana ambao kutokana na kukosa elimu hii ya jinsia, wanaamini kuwa wao kama watoto hawawezi kupata mimba, mwandishi anamtumia muhusika Joti anapowaambia rafiki zake, “Mara moja tu, hakuna mimba sisi watoto.” {Uk. 16}

Mwandishi hakuishia tu kuonesha madhara ya kukosa elimu hii ya jinsia, kwa upande mwingine ameonesha faida za elimu hii ya jinsia na ukimwi kwa vijana, mwandishi anaonesha kuwa, vijana waliopata elimu hii, huwasaidia sana kupambana na kujizuia na vishawishi vya kingono kutokana na uelewa waliokuwa nao, kwa mfano mwandishi anamtumia muhusika Anna, ambaye kutokana na mafunzo aliyopewa na wazazi wake yanamsaidia sana kupambana na kujizuia na vishawishi hivyo kutokana na kufahamu madhara ya kushiriki ngono kabla ya wakati, hili mwandishi analithibitisha akimtumia muhusika Anna anaposema, “...Hujui kama kuna madhara mengine. Hujui magonjwa ya zinaa wewe: hujui kisonono, kaswende na mengine kedekede. Haya hata UKIMWI hujui?”  {Uk. 25}

Hivyo mwandishi anashauri, elimu hii ya jinsia na UKIMWI, isitolewa kiubaguzi, itolewe kwa watu wote kwani kila mtu yuko katika hatari ya kuambukizwa virusi vya UKIMWI, mwandishi anaonesha namna ambavyo vijana wanateketea kwa kubaguliwa kwao kupewa elimu hii, rejea ukurasa wa 1-2, Mtambaji anaposimulia, “Wakubwa wakaandika mabuku kupeana habari. Wakabandika mabango kupeana tahadhari, lakini watoto wakateketea kwa kukosa habari zozote za kuwaokoa.”

Mwandishi anaonesha kuwa, kama vijana wangeelimishwa kuhusu madhara ya kufanya mapenzi kabla ya wakati, namna ya kujilinda, basi wasingetummbukia katika janga hili, mwandishi anathibitisha kwa kumtumia muhusika  Suzi anaposema, “Naapa kwa Mungu wangu, mimi na Joti tungepata bahati ya kuelimishwa, tusingetumbu...tusi...(Anaanguka chini.)” {Uk. 36}


(b) Dhamira ndogo ndogo
1.     Ukosefu wa elimu
Dhamira hii inajitokeza katika tamthiliya, mwandishi anaonesha kuwa ukosefu wa elimu ya namna ya kupambana na Ukimwi unaifanya jamii kushindwa kulikabili gonjwa hili, ukosefu wa elimu unawafanya wengine kuamini ugonjwa huu ni wa kurogwa, wengine wanaamini ni ugonjwa unaletwa na mizimu na hata wengine kudhani ni majini.

2.     Mapenzi na ndoa
Suala la mapenzi na ndoa pia limepewa nafasi katika tamthiliya hii, tukianza na suala la mapenzi, mwandishi anajadili mapenzi ya namna mbili, mapenzi ya dhati na mapenzi ya ulaghai.
(a)  Mapenzi ya dhati
ü Baba Anna kwa familia yake
ü Mjomba kwa Suzi
ü Anna kwa wazazi wake
ü Anna kwa Suzi
ü Suzi kwa Joti
(b) Mapenzi ya ulaghai
ü Joti kwa Suzi
ü Joti kwa Chausiku
ü Chausiku kwa Joti

     

3.     Malezi kwa vijana
ü Mwandishi pia amegusia suala la malezi kwa watoto, mwandishi anaonesha kuwa, malezi bora kwa mtoto ni malezi ya wazazi wote wawili, yaani baba na mama, na anapokosekana mzazi mmoja huweza kumuathiri mtoto, katika tamthiliya hii tunamuona Suzi akilelewa na mama peke yake bila baba hali hii inachangia mtoto kuingia katika matatizo, hili linathibitishwa na mwandishi akimtumia muhusika Mama Suzi anaposema, “Kila siku ninasema mwanangu mdogo, mwanangu ni mtoto mzuri, leo Suzi unanifanyia hivi? Hivi baba yako angekuwepo ungefanya hivi? Ah Suzi, ungefanya?” {Uk.31}
ü Katika suala hili la malezi, mwandishi anatuambia kuwa kuwa, mzazi ndiyo mwalimu bora kwa malezi mema ya mtoto,rejea ukurasa wa 11, Mjomba na Baba ANNA wanaposema, “Mzazi ndiye mwalimu wa kwanza...Na ndiye bora.” {Uk. 11} hivyo wazazi wawafundishe vema watoto wao, lakini wazazi wasipofanya hivyo, walimwengu watawafundisha na kwa kawaida walimwengu hufundisha katika upotofu, rejea ukurasa wa 10-11, Baba Anna anaposema, “Dunia imeharibika bwana. Mzazi usipomfunza, walimwengu watamfundisha tena sasa si maadili mema bali njia potofu.” {Uk.10-11}

ü Mwandishi pia anaonesha kuwa, ili watoto/vijana wawe na maadili mema, wazazi wanatakiwa kukaa na watoto wao kuwaelimisha mambo mbalimbali ambayo yanaweza kuwa na madhara kwao kama alivyofanya Baba Anna na mke wake, rejea ukurasa wa 10 Baba Anna anapowaambia wenzake, “Hilo ndilo mie nililofanikiwa mwenzenu. Nimemwambia mama Anna akae na mabinti zake name nikae na vijana wangu wa kiume. Tumefanya kazi hiyo kwa makini sana. Tumewaelimisha juu ya madhara ya tabia hiyo kwao binafsi na kwetu sote. Hatukubakiza kitu.” {Uk. 10}


4.     Usaliti
Usaliti ni dhamira nyingine inayojitokeza katika tamthiliya hii, kwa mfano mwandishi anaonesha usaliti unaofanywa na Baba Joti kwa mke wake, Baba Joti anaisaliti ndoa yake kwa kuanzisha uhusiano wa kimapenzi na mwanamke mwingine, hili linathibitishwa na Mama Anna anaposema, “Lakini leo nimefika kikomo. Ndiyo mwisho wa kumvumilia huyu nguru anayeichimba ndoa yangu.” {Uk. 7}

Usaliti mwingine, tunaona kwa Joti, pamoja na kwamba Joti anakuwa na mahusiano ya kimapenzi na Suzi anaamua kumsaliti na kuanzisha mahusiano na wanawake wengine, mwandishi analithibitisha hili akimtumia muhusika Suzi anaposema, “Ndiyo maana mie nilikuwa nakataa Joti. Nishaambiwa kwamba unawasichana wengi shuleni na mtaani kwetu.” {Uk. 21}

Usaliti mwingine unajitokeza kwa Joti na Chausiku, mwandishi anaonesha kuwa Joti pamoja na kuwa na mahusiano na Chausiku anamsaliti Chausiku kwa kuwa na mahusiano na wasichana wengine, Joti anapewa vitu na Chausiku naye anawapa wanawake wengine, rejea ukurasa wa  22, Chausiku anaposema, “Toka hapa. Nimesikia habari zako. Kila msichana unamtaka tu. Mie nakununulia fulana ya mazoezi wewe unahonga kinyago chako kile. Bisha...Nikikupa hela ya kununua peni we unanunulia bazooka visichana vyako.” {Uk. 22} lakini si Joti tu ndiye anamsaliti mwenzake, mwanandishi anatuonesha kuwa, hata Chausiku pia, anamsaliti Joti kwa kuwa na mahusiano na wanaume wengine, rejea ukurasa wa 22-23, Mwarami anapomwambia Joti, “Sasa ndiyo kuparamia mpaka wasichana wakubwa wa mtaani? Fikiri juu ya Chausiku, Yule msichana mjuvi wa mji ambaye pia anachukuliwa na Yule mpemba muuza duka.” {Uk. 22-23}

Tukigeukia katika uhalisia wake, suala la usaliti katika ndoa au mapenzi bado ni tatizo kubwa sana katika jamii yetu, wanandoa wanasalitiana, wapenzi wanasalitiana tabia hii ya usaliti huwa ni kichochea kikubwa sana kwa watu kuambukizana virusi vya ukimwi, kama tunavyoona kwa Joti. Hivyo jamii iache usaliti.

5.     Athari za utandawazi
Mwandishi pia amejadili suala la utandawazi na athari zake, mwandishi anaonesha namna utandawazi unavyochangia kwa kiasi kikubwa kuharibu tabia na maadili ya watoto na vijana, kwa mfano tunawaona akina Joti, Jumbe, Choggo na Mwarami wanajiingiza katika mahusiano ya kingono wakiwa watoto wadogo kutokana na kuathiriwa na video za ngono (sinema za X) wanazozitazama mtaani, mikanda hii ya ngono imekuwa rahisi sana kupatikana kutokana na utandawazi.

6.     Athali za ukoloni na ukoloni mambo leo
Suala la ukoloni na ukoloni mambo leo pia limepewa nafasi katika tamthiliya hii, mwandishi anaonesha namna  wakoloni walivyoharibu utamaduni wetu kwa kuuita ushenzi na hata tulivyopata uhuru, viongoni wetu wakaendelea kushikilia mawazo hayo potofu ya kikoloni ambayo kwa kiasi kikubwa tunaangamia wenyewe, hili mwandishi analithibisha akimtumia Mtambaji anaposema, “Mila zetu hazikukataza kutoa mafunzo ya elimu ya jinsia...Wakoloni na vibaraka wao ndio wanaostahili kulaumiwa wakoloni walipiga vita jando na unyago wakidai eti ni ushenzi.” Mtambaji anaendelea kutuambia tena, “Viongozi wetu nao wakaendeleza mawazo hayo hata baada uhuru bila kutambua kuwa wanajiua wenyewe.” {Uk. 13-14}

7.     Nafasi ya mwanamke katika jamii
ü Mwanamke amechorwa kama mlezi wa familia, mwandishi anatuonesha namna ambavyo mwanamke anakuwa mlezi mzuri wa familia, anaangaika hapa na pale kuhakikisha mtoto au watoto wake wanapata mahitaji yote muhimu kama vile chakula, mavazi na hata elimu, rejea ukurasa 30, Mama Suzi anaposema, “Mimi ninahangaika kukusomesha, wewe unanifanya hivi...Mama yako nimeungua viganja kwa kupika vitumbu ili mwanangu usome.” {Uk. 30}

ü Mwanamke amechorwa kama mtu mwenyemsimamo, mwandishi anamtumia muhusika Anna kumuonesha mwanamke kama mtu mwenye msimamo katika maamuzi yake, tunamuona Anna pamoja na kusumbuliwa mara kwa mara na Mwarami kumtaka kimapenzi bado anashikilia msimamo wake ule ule wa kumkatalia, hata watu wazima wenye uwezo kipesa wanapomtaka Anna bado Anna anaonesha kutoyumba kimimamo kwa kuwakatalia. Rejea wimbo anaoimba Anna ukurasa wa 27,
                             “Anna Anna Anna mie niacheni mie x2
                              Msichana mdogo bado nasoma niacheni mie.
                              Muda wangu kufanya hayo haujafika mie.
                               Pesa zenu, na lifti zenu niacheni mie.
                               Anna Anna Anna mie niacheni x2”

ü Mwanamke amechorwa kama mtu anayepinga mabadiliko katika jamii, mwandishi anatuonesha kuwa mwanamke ni mtu asiyependa mabadiliko katika jamii, asiyependa kwenda na wakati, dunia inabadilika jamii inatakiwa kuwaelimisha vijana wao kuhusu elimu ya jinsia na mahusiano ,Mama Suzi anapinga, rejea Mama Suzi anaposema, “Tena ishia hapo hapo kaka! Huko si kunifundishia mwanangu umalaya? Umfunze mwanangu habari za ngono ilitoka wapi hiyo? {Uk. 9}

ü Mwanamke amechorwa kama mtu asiye na msimamo, mwandishi anatuonesha kuwa, mwanamke ni mtu asiye na msimamo katika maamuzi yake, mwandishi anamtumia Suzi, kuijadili nafasi hii, richa ya Suzi kuamua kuachana na Joti na hata anapogundua kuwa Joti anamahusiano na wanawake wengine bado anakubali kuendelea naye. (Rejea uk. 17 na 21)
ü Vile vile, mwandishi amemchora mwanamke kama chombo cha starehe, anamtumia muhusika Joti ambaye anawatumia wanawake ili kujistarehesha kingono, lakini pia tunaona namna watu wanavyotumia pesa na vitu vya thamani ili kuwarubuni wasichana wapate kukidhi mahitaji yao ya kingono. {rejea ukurasa 27}

ü Mwanamke amechorwa kama mtu asiye na elimu juu ya mambo ya jinsia na ukimwi, katika kuilezea nafasi hii, mwandishi anamtumia muhusika Mama Suzi, ambaye anaoneka kutokuwa na ufahamu mzuri juu ya masuala ya UKIMWI, kwa mawazo yake anaamini kuwa ugonjwa wa UKIMWI ni ugonjwa unaowahusu watu wakubwa tu, na watoto hawawezi kuambukizwa jambo ambalo si sahihi. Hata katika jamii yetu, wapo watu wanaoamini kuwa ugonjwa huu wa UKIMWI huwakumba watu wazima watoto na watu walio katika ndoa hawawezi kuambukizwa virusi vya ukimwi jambo ambalo si kweli. Hivyo jamii inatakiwa kuelimishwa sana kuhusu ugonjwa huu.

Mfano wa maswali unayoweza kuulizwa sehemu hii
1.     Taja maadui sita na fafanua jinsi waandishi wa tamthiliya mbili kati ya ulizosoma walivyojitokeza kupambana na maadui hao.
2.     Waandishi wa tamthiliya wamemchora mwanamke katika sura tofauti. Thibitisha kauli hii kwa kutumia waandishi wawili (2) wa tamthiliya mbili (2)ulizosoma.
MIGOGORO
Migogoro ni hali ya kutoelewana baina ya pande mbili, unaweza kuwa mgogoro kati ya mtu na mtu, mtu na kikundi cha watu, kikundi kimoja na kikundi kingine cha watu au unaweza kuwa mgogoro wa mtu na nafsi yake. Katika tamthiliya hii, mwandishi ameweza kuibua na kuonesha migogoro mbalimbali ambayo kwa kiasi kikubwa migogoro hiyo imeweza kusaidia katika ujenzi wa dhamira mbalimbali zilizoweza kujitokeza katika kazi hii, migogoro iliyojitokeza katika tamthiliya hii ni:

ü Mgogoro kati ya Mama suzi na mwanaye,(Suzi) chanzo cha mgogoro ni Mama Suzi kukuta kasha la vidonge vya kuzuia mimba kwenye mfuko wa sketi ya Suzi, mgogoro unakua zaidi Mama Suzi kuamua kumuadhibu kwa kumchapa Suzi hadi anapotokea Mjomba na Baba Anna, kuamulia mgogoro huo na kushauri jambo la msingi ni kumpa elimu ya jinsia na si kutumia ukali na viboko, kama ambavyo Baba Anna anasema, “Watoto wajazwe elimu, waone uchafu na hatari ya kufanya haya. Siyo kuwatia hofu tu. Je leo ukifa ama kulazimika kuwa mbali nawe? Si atafanya tu maana mtia hofu hayupo?” {Uk. 13}

ü Mgogoro kati ya Mjomba na Mama Suzi, chanzo cha mgogoro ni kitendo cha Mjomba kumshauri Mama Suzi kuacha kumuadhibu Suzi na badala yake apewe elimu ya jinsia na mahusiano ya kimapenzi jambo linalopingwa na Mama Suzi na hivyo kuibua mgogoro. {Rejea ukurasa wa 8-14}


ü Mgogoro kati ya Suzi na Joti, mgogoro huu unaibuka baada ya Suzi kupigwa na mama yake sababu ya vidonge vya kuzuia mimba alivyopewa na Joti, mgogoro huu unafikia hatua ya Suzi kuamua kuachana na Joti, suluhisho la mgogoro huu, wanaamua kurudiana na kuendelea na uhusiano wao. (Rejea uk. 17 na 21)

ü Mgogoro kati ya Mwarami na rafiki zake yaani Jumbe, Joti na Choggo. Chanzo cha mgogoro ni kitendo cha Mwarami kutokuwa na uhusiano wa kimapenzi na wasichana, hatua inayosababisha kumtishia kumfukuza katika kundi lao, rejea ukurasa wa 24, Jumbe anapomwambia Mwarami, “Sasa bwana hapa kwenye grupu letu hatutaki tabia hiyo ya ushamba. La sivyotutakutoa umemba.” Suluhisho la mgogoro huu ni Mwarami kuamua kumshawishi Anna kimapenzi hata hivyo juhudi zake zinagonga mwamba.


ü Mgogoro kati ya Mama Joti na Mwanamke anayedhani anaingilia ndoa yake, Mama Joti anaona suluhisho la mgogoro huu ni kununua kanga zenye maneno ya vijembe ili kumpasha na kumuumiza roho, Rejea Mama Joti anaposema, “Lakini leo nimefika kikomo. Ndiyo mwisho wa kumvumilia huyu nguru anayeichimba ndoa yangu...Ngoja kwanza nimpashe najua litamuuma tu.” {Uk. 7}

ü Mgogoro mwingine ni kati ya Chausiku na Joti, chanzo cha mgogoro huu ni baada ya kugundua kuwa Joti anamahusiano ya kimapenzi na wasichana wengine, mgogoro unafikia hatua ya Chausiku kumtishia kumdhuru Joti, kama anavyosema, “We usinifanye mie bwege mwenzio...wewe ndiyo unajigonga gonga. Wewe na visichana vyako hivyo nitawachoma moto mie! Nyie hamnijui, ohoooo!” {Uk. 22}

ü Mgogoro kati ya ukale na usasa, huu ni mgogoro mwingine unaojitokeza katika tamthiliya, mwandishi anaonesha mgogoro kati ya watu wanaokumbatia mambo ya kale, mambo yaliyopitwa na wakati na wale wanaotaka mabadiliko katika jamii, mwandishi anawatumia wahusika, Mama Suzi na Baba Joti kama watu wanaokumbatia mambo ya kale na kwa upande mwingine anawatumia wahusika, Mjomba, Baba Anna na Mama Anna kama watu wanaotaka mabadiliko katika jamii, wanataka ukuta unaowatenga watoto na wazazi wao wasipate elimu ya jinsia ubomolewa, mwandishi anaonesha kuwa, kukumbatia mambo ya kale kunaweza kuleta madhara kwa vijana kama madhara ya kupata mimba kwa Suzi, rejea Suzi anaposema, “Mama hakuwa radhi kuachana na utamaduni wa kale wa kuweka ukuta baina ya wazazi na watoto katika kujadili mambo haya. Haya ndiyo madhara yake.” {Uk. 36}

ü Mgogoro wa Suzi na nafsi yake, chanzo cha mgogoro huu ni kitendo cha kuambiwa na mama yake kuwa shangazi yake ataenda kumpima mimba, Suzi anaona suluhisho la mgogoro huu ni kutokubali kwenda kupimwa mimba na shangazi yake na badala yake kumtafuta mwanaume anayehusika na mimba hiyo (Joti)  kuzungumza naye, rejea Suzi anaposema, “Oh Mungu wangu! Nifanye nini sasa? Siwezi kumruhusu shangazi akanipime...oh, nifanye nini mie! Nimtafute Joti, lazima niongee naye.” {Uk. 31}


ü Mgogoro mwingine unaojitokeza ni mgogoro wa Suzi na nafasi yake kama ameambukizwa virusi vya Ukimwi au la, chanzo cha mgogoro huu ni baada ya Suzi kugundua kuwa ana mimba na kijana aliyempa hiyo mimba ameathirika na virusi vya ukimwi, rejea Suzi anaposema, “Na mie Suzi nina mimba, mimba ya Joti. Kasha ina maana na mie nina ukimwi?” {Uk. 36}

UJUMBE
Ujumbe ni funzo analolipata fanani anaposoma ama kusikiliza kazi za fasihi, pamoja na ujumbe pia kuna maadili mbalimbali hupatikana, katika tamthiliya hii kuna mafunzo mbalimbali ambayo msomaji wa kazi hii anaweza kuyapata, mafunzo hayo ni kama:

ü Elimu ya jinsia na ukimwi ni muhimu kwa vijana ili kuwanusuru vijana na mimba za utotoni(mimba zisizotarajiwa) na maambukizi ya virusi vya ukimwi.
ü Ukimwi hauchagui rika, mwandishi anatupa ujumbe kuwa gonjwa hili la UKIMWI hauchagui mtu, kila mtu anaweza kuupata, kama tunavyoona kwa Fausta na Joti, ni watoto wadogo lakini wanaathirika na virusi vya ukimwi na kusababisha vifo vyao.

ü Asiyefunzwa na mama yake, hufunzwa na ulimwengu, hili ni funzo linguine tunalilipata katika tamthiliya, mwandishi anatufundisha umuhimu wa wazazi kuwafundishi watoto wao maadili mema na si kuwaacha watoto wakajifunza wenyewe mtaani, wakiwaacha hivyo, huko hujifunza mambo yasiyofaa, tunaona kwa Suzi, Joti, Mwarami, Choggo, Jumbe, wazazi wao hawakuwafundisha elimu ya jinsia na mahusiano watoto wakajifunza wenyewe mambo machafu na hataimaye yakawaletea madhara.


ü Wazazi ndiyo walimu bora kwa malezi bora na maadili mema kwa watoto wao. Mwandishi anaendelea kutufundisha kuwa, ili vijana wetu wawe na tabia njema, mzazi ni mwalimu bora kabisa anayeweza kumfundisha mtoto wake vema, rejea mwandishi akimtumia muhusika Baba Anna anaposema, “Dunia imeharibika bwana. Mzazi usipomfunza, walimwengu watamfundisha tena sasa si maadili mema bali njia potofu.”

ü Kinga ni bora kuliko tiba. Ni vizuri jamii ikajikinga na magonjwa mbalimbali, kuliko kutojikinga na baadaye kuanza kutafuta tiba, tiba huwa gharama sana kuliko kujikinga, tunamuona Baba Joti akitumia gharama kubwa kutafuta tiba  ya mtoto wake, kama ambavyo mwandisha anasema, “Mtani ushauza rasilimali zako kuuguza mtoto. Ushajitia umskini kwa kuhangaika...” {Uk. 34} Hivyo basi ni vema jamii ikaamua kujikinga dhidi ya matatizo mbalimbali kwani matatizo hayo pindi yanapokukumba huwa ni gharama sana kuyatatua na wakati mwingine matatizo mengine huwa hayana tiba kama tunavyoona katika ugonjwa wa UKIMWI.

ü Ngono zembe ni chanzo cha maambukizi ya virusi vya ukimwi na mimba zisizotarajiwa, Tunamuona Joti akiambukizwa virusi vya ukimwi kutokana na kushiriki ngono zemba, vilevile tunamuona Suzi akipata mimba na hata kuwa katika wasiwasi wa kuambukizwa virusi vya UKIMWI kutokana na kushiriki ngono zemba. (Rejea ukurasa wa 4 na 34)

Mafunzo mengine tunayoyapata katika tamthiliya hii ni pamoja na:
ü Jamii inatakiwa kubadilika ili kwendana na mabadiliko katika jamii.
ü Mila na desturi zilizopitwa na wakati hatuna mudi kuachana nazo
ü Huwezi kumtambua mtu aliyeathirika na virusi vya ukimwi kwa kumtazama kwa macho tu. Uk. 4-5
ü Vijana waelimishwe namna ya kukabiliana na changamoto za utandawazi.
ü Utandawazi ni chanzo cha mmong’onyoko wa maadili ya vijana.
ü Malezi bora ni muhimu kwa watoto/vijana ili kuwa na maisha bora baadaye.
ü Majuto ni mjukuu, tunamuona Suzi akijuta kutokana na kutopata elimu ya jinsia na hivyo kujikuta akitumbukia katika matatizo.

MATUMIZI YA LUGHA
Mwandishi ametumia lugha ya kawaida, sentensi fupifupi na inayoeleweka kwa urahisi,pamoja na hayo mwandishi pia ametumia lugha ya kisanaa yenye mbinu mbalimbali za kisanaa kama vile nahau na tamathari za semi.

(a)  Matumizi ya methali
ü “Mzazi usipomfunza, walimwengu watamfundisha.” Uk.
ü “Shukrani ya punda mateke.” {Uk. 19}

(b) Matumizi ya misemo na nahau
ü Shoga, mtakatifu wa kwenye mwanga si lazima awe mtakatifu gizani. {Uk. 4}
ü “Kakanyaga nyaya.” {Uk. 4}
ü “Potelea kwao...” uk. 9
ü “Makapera kibao, mume wangu wa nini. Uk. 7
ü “Wembamba wa reli treni inapita, uk 6
ü Kifua simkingii, maana siwi naye. Uk 6
ü “Kwa mashairi nimekuvulia kofia siku nyingi.” Uk.6
ü  “We pita juu mie nipite chini...”uk 19
ü Mbona umetuanika juani. Uk 16
ü “Hakikisha ndege mjanja ananasa katika tundu bovu.” Uk. 24

(c)  Matumizi ya taswira/lugha ya picha
ü Dubwana, Manaa yake ni kitu au mtu mwenye umbo kubwa lisilo la kawaida au la hovyo hovyo, mwandishi ametumia neno dubwana kitaswira kuufananisha ugonjwa wa Ukimwi sawa na jambo linalotisha, kuogopesha. (Rejea ukurasa wa 1-2)
ü Gizani, gizani ni mahali pasipokuwa na mwanga, hivyo mwandishi ametumia neno giza, akimaanisha kukosa maarifa au kutokuwa na ufahamu ya jambo fulani, kwa kifupi kukosa elimu,  Rejea mtambaji anaposema, “Kisiwa kizima kipo gizani...watoto ndio kabisa. Wapo katika giza nene.” {Uk. 13}

(d) Matumizi ya tamathali za semi.
(i)                Tashibiha, hizi ni tamathari ambazo hulinganisha vitu kwa kutumia viunganishi kama, mfano wa, sawa na, mithili ya, kama vile. N.k. baadhi ya tashibiha zinazojitokeza katika tamthiliya hii ni:
ü “Wewe nawe unakuwa nyuma nyuma kama koti.” Uk. 4
ü “Shoga mbona unakuwa mgumu kama mpingo?” uk. 5
ü “Watu walipukutika, wakapukutika kama majani ya kiangazi.” Uk.1
ü “Lile Dubwana limetanda kama utando wa buibui.” {Uk.13}
ü “Miti inayoungua kama mabua.” Uk. 6

(i)                Sitiari, hizi ni tamathari za semi ambazo hulinganisha vitu bila kutumia viunganishi, mfano wa tamathali zilizotumika ni pamoja na:
ü “We mbwa mweusi.” Uk. 8
ü “Nyoka wee.” Uk.9

(ii)             Mjalizo, hii ni aina ya tamathali za semi ambazo msanii/mwandishi huitumia kutaja vitu au mambo yaliyo katika orodha bila kutumia viunganishi. Mfano:
ü “...Lakini soma maneno yake. Yamejaa kejeli, ushari, uchimvi, kusengenyana na kufumbiana mafumbo ya kila aina.” Uk. 6

(iii)           Nidaa, hizi ni tamathali za semi, zinazoonesha hali ya kushangaa au kushangazwa na jambo Fulani, mfano wa tamathali hizi ni:
ü “Ai, ai, lahaula lakwata...weye, hiki kitoto?” {uk. 9}
ü “Oi, oi, oi, toba! Kile si kitoto kama cha kwangu...” {uk.10}

(iv)            Takriri, hii ni hali ya kurudiarudia maneno, neno, silabi au sauti zinazolingana katika kazi ya fasihi ili kusisitiza au kutia mkazo jambo fulani. Mfano wa takriri zinazojitokeza katika tamthiliya hii ni:

ü “Watu walipukutika, wakapukutika kama majani ya kiangazi.     Wakapukutika.” Uk. 1
ü “Waongo! Waongo wakubwa.” Uk. 3
ü “ Vifo vikawazoa, vikawazoa...vikawazoa.” uk. 2
ü “Piga domo, piga doma, nikashinda.” Uk. 16

(v)              Tanakali sauti Hii ni aina ya tamathali ambayo sauti ya kitu fulani huigwa ili kwa lengo la kuburudisha au kuipa dhamira uzito falani. Mfano wa tanakali sauti zilizotumika katika tamthiliya hii ni:
ü “Wacha moyo unipwite pwi,pwi,pwi...” uk.16

(vi)            Tashititi Hii ni aina ya tamathari ya semi ambayo mtu huuliza swali huku jibu lake akilifahamu, mfano wa tashititi zinazojitokea katika tamthiliya hii ni:
ü “Huyu ni Suzi kweli au nani?” uk.15

Mfano wa maswali unayoweza kuulizwa sehemu hii
1.     Lugha ni kipengele muhimu sana kwa mwandishi katika kufikisha ujumbe wake kwa jamii. Jadili kauli hii kwa mifano toka katika tamthiliya mbili ulizosoma.
MTINDO NA MUUNDO
(a)  Mtindo
Mtindo ni jinsi msanii anavyotumia ufundi, umahiri na hisia zake katika kutenda au kueleza jambo fulani katika kazi ya fasihi, na mtindo ndiyo huweza kumtofautisha msanii/mwandishi mmoja na mwandishi mwingine. Mtindo hutumika kuipamba kazi ya fasihi, baadhi ya mitindo nayotumika katika kazi hii ni pamoja na:

ü Matumizi ya hadithi ndani ya tamthiliya
Mwandishi ametumia mtindo wa hadithi ambao ni utanzu wa fasihi simulizi ndani ya tamthiliya, mtindo huu unajidhihirisha ukurasa wa kwanza, Mtambaji anapoanza kusimulia hadithi anaposema, “Paukwa” na hadhira inaitikia “Pakawaaaaaaa” na Mtambaji anaendelea, “Hapo zamani za kale paliondokea kisiwa kimoja...” {Uk. 1} Ni utanzu wa hadithi pekee ndiyo huwa na mwanzo wa namna hiyo.

ü Matumizi ya wimbo/shairi ndani ya tamthiliya
Mwandishi pia ametumia wimbo kuipamba kazi yake, wimbo unajitokeza ukurasa wa 27 Anna anaimba wimbo unaowataka wanaume wanaomtaka kimapenzi kuacha kumfuatafuata, muda wake wa kujihusisha na mahusiano ya kimapenzi haujafika bado mwanafunzi.                        
                              “Anna Anna Anna mie niacheni mie x2
                              Msichana mdogo bado nasoma niacheni mie.
                              Muda wangu kufanya hayo haujafika mie.
                               Pesa zenu, na lifti zenu niacheni mie.
                               Anna Anna Anna mie niacheni x2”

ü Matumizi ya lugha ya majibizano/dialojia na masilmulizi
Kama ilivyo ada, mtindo wa lugha unaotumika katika tamthiliya, kwa asilimia huwa ni mtindo wa majibizano, yaani dialojia. Hivyo basi hata katika tamthiliya hii, mwandishi kwa kiasi kikubwa ametumia mtindo wa majibizano na kidogo ametumia masimulizi, (Rejea masimulizi ya Mtambaji ukurasa wa 1-2, 3-4, na 36)

ü Matumizi ya nafsi zote tatu
Pia nafsi zote tatu zinajitokeza katika tamthiliya hii,
ü Nafsi ya kwanza, mfano,Mimi nawashangaa... {Uk. 6} Najua litamuuma tu (uk.7), Tumebomoa ghala imara...” {Uk. 6}
ü Nafsi ya pili, mfano, “Utamaliza kanga zilizoandikwa kila aina ya maneno...”
            Wewe unamwona Fausta alikuwa mdogo?
ü Nafsi ya tatu, mfano, ...alikufa kwa ukimwi” uk. 9, atakutafuta tu mwenyewe.” (uk 17), “Wanashindwa kutofautisha kati ya puto na kondomu.” (Uk. 13)

ü Matumizi ya picha, mwandishi pia ametumia michoro mbalimbali inayoonesha matendo/matukio mbalimbali ya wahusika, picha hizi zimesaidia sana kuipamba na kuipendezesha kazi yake, picha hizo zinapatikana ukurasa wa 3,5,8,11,17,20,23,27, 29 na 35.

(a)  Muundo
Muundo ni mfuatano wa masimulizi au visa katika kazi ya sanaa ya fasihi, hivyo basi.muundo wa tamthiliya hii ni wa moja kwa moja, yaani visa vyake vimepangwa kuanzia kisa cha kwanza , kati hadi mwisho, katika kuvipanga visa vyake, mwandishi ameigawa kazi yake katika sehemu sita, ambazo amezipa majina, Sehemu ya kwanza, Sehemu ya Pili, ya Tatu, ya Nne, Tano na Sehemu ya Sita.

Sehemu ya kwanza.
Mtambaji anasimulia habari za Dubwana(Ukimwi), anasimulia namna wakubwa wanavyoelimishana namna ya kujilinda na ugonjwa huo, huku wakiwaacha watoto wakiangamia kwa kukosa elimu ya jinsia na ukimwi.

Sehemu ya Pili
Hapa mwandishi anatuonesha nyumbani kwa Mama Suzi, Mama Suzi na Mama Joti wanapeana habari za kifo cha Fausta kilichosababishwa na ukimwi, Mama Suzi anakuta kasha la vidonge kwenye mfuko wa sketi ya Suzi wakati akifua jambo linalozua mgogoro kati ya Suzi na mama yake, Mjomba na Baba Anna wanamshauri Mama Suzi kuacha kutumia ukali na badala yake anatakiwa kumpa elimu ya jinsia binti yake ili ajitambue jambo linalopingwa vikali na Mama Suzi.

Sehemu ya Tatu
Hapa mwandishi anatuonesha mtaani, Joti anakutana na Suzi, Suzi anaamua kuachana na Joti kwa sababu ya vidonge vya kuzia mimba alivyopewa na Joti kumsababishia kupigwa na mama yake. Joti anawasimulia wenzake namna alivyofanikiwa kumpata Suzi, Joti, Jumbe, Choggo na Mwarami wanaenda mtaani kuangalia sinema za X.

Sehemu ya Nne
Tukio linatendeka njiani, Joti na Suzi wanakutana, Suzi anamlaumu Joti kwa kuwa na mahusiano ya kimapenzi na wasichana wengine, wanaamua kurudisha uhusiano wao, Joti anaanza kujisikia vibaya, Jumbe anaamua kumpeleka nyumbani, Mwarami anaonekana akimshawishi Anna amkubalie ombi lake la kuanzisha mahusiano ya kimapenzi, Anna anaonesha msimamo anamkatalia, mwandishi pia anatuonesha namna Anna anavyoshinda vishawishi vya kingono.

Sehemu ya Tano
Tukio linatendeka chumbani kwa Suzi akiwa na Anna, Suzi anajisikia vibaya, anahisi huenda ana mimba, anataka kuitoa, rafiki yake Anna anamshauri kuachana na mpango huo kwani ni hatari, anaamua kwenda kwa Joti kuzungumza naye suala hilo.

Sehemu ya Sita
Hii ni sehemu ya mwisho, mwandishi anatuonesha nyumbani kwa Baba Joti, tunaona namna Baba Joti alivyoangaika kwa waganga mbalimbali kutafuta tiba ya Joti bila mafanikio, mwisho wanaamua kumpeleka hospitali, huko wanapata wajibu kuwa Joti amethirika na virusi vya ukimwi, Jirani anamshauri Baba Joti kumpeleka Joti kwa mganga mwingine, Mjomba anamshauri Baba Joti kuachana na mpango huo kwani ugonjwa alionao Joti hauna tiba wala dawa. Suzi anawasili kwa akina Joti anagundua Joti ana ukimwi, Joti anafariki dunia, Suzi anakuwa na wasiwasi kama naye atakuwa ameambukizwa virusi vya ukimwi, anabaki akijutia kwa kukosa elimu ya jinsia na ukimwi.  Na mchezo unaishia hapo.

BOFYA HAPA KUENDELEA
Share:

CLIC THE IMAGE SUBSCRIBE NOW

CLIC THE IMAGE SUBSCRIBE NOW
Bofya Picha Hiyo Hapo Juu Kisha Subscribe Channel Yetu ya Online Class Utapata Offer ya Kutumiwa Vitabu vyaasomo Yote Buree Kupitia Whatsap Yako

FUNDISHWA SASA NA TEACHER HASSAN LEMUNJE KWA NJIA YA MTANDAO KWA GHARAMA NAFUU.

FUNDISHWA SASA NA TEACHER HASSAN LEMUNJE KWA NJIA YA MTANDAO KWA GHARAMA NAFUU.
Popote ulipo bofya hapa uanze kufundishwa na Teacher Hassan Lemunje. Utatumiwa notes, voice notes za maelekezo kwa lugha nyepesi, pamoja na huduma ya solving ya mitihani yote ya Necta pamoja na Mock Regions sambamba na mbinu mbalimbali za kujibu na kufaulu mitihani Yako. Huduma hii ni kwa wanafunzi wa Level zote wenye kutumia WhatsApp. Piga Sasa uweze kuunganishwa (0622548220/076910272).

BLOGS AND GRAPHICS DESIGN; CONTACT US

Search This Blog

About Me

My photo
DAR ES SALAAM, MAPINGA BAGAMOYO, Tanzania
HASSAN AMONI LEMUNJE born in 31 August,1998. He is Professional Teacher as he teach various schools in Tanzania includes Mlali Sec school, Hijra Seminary, Jamhuri Sec school and currently at Baobab Sec school, an author, public speaker, Translator, Interpreter, and editor of various books, dissertations, term papers, research proposals, and articles.��His life purpose: To use my God-given talents to inspire, empower and become a good role model by supporting others to develop their potentials to the fullest and leave the world a better place than I found it & Yupo hapa kwaajili ya kukuletea masuala yote ya kitaaluma Nchini Tanzania. Pia anapatikana FACEBOOK TWETER na INSTAGRAM(@TeacherHassanLemunje) Contact me +255622548220 +255769010272